Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi wa afya ngazi ya kata katika Jimbo la Nanyumbu?
Supplementary Question 1
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Wilaya ya Nanyumbu ina kata 19 ambazo hazina nyumba za watumishi na ina vituo vya afya viwili ambavyo havina nyumba za watumishi. Kwa majibu haya ya Serikali kwamba imetengwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili maana yake itatumia miaka 10 kukamilisha nyumba hizi.
Mheshimiwa Spika, swali; sasa hivi tunajadili bajeti ya Waziri Mkuu, ningependa kufahamu ni kiasi gani kimetengwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hizi za ukosefu wa nyumba za watumishi wa afya katika jimbo langu?
Mheshimiwa Spika, pili, je, Serikali haioni kwamba wakati umefika sasa tuka-engage private sector au tukashirikiana na taasisi (National Housing, TBA, JKT) ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba hizo za watumishi kule vijijini ili kukabiliana na changamoto hii? (Makofi)
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Ally Yahya kwa kuwasemea watumishi wa Jimbo la Nanyumbu na kule waliko watumishi wanafarijika sana kuona Mheshimiwa Mbunge anawapambania.
Mheshimiwa Spika, Serikali tumeshafanya tathmini, tuna hitaji la nyumba hizi zaidi ya 25,000, lakini tayari tumeshafanya mpango wa utafutaji wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 241 kwa ajili ya kuanza kujenga ujenzi angalau wa nyumba 2,000 zile three in one kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika, swali la pili Mheshimiwa Mbunge kwanza ni ushauri wa Kamati ya TAMISEMI, tulipata ushauri lakini pia tumepata mwongozo kutoka Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwamba sasa tufanye engagement kwa private sector ili nao waweze kuingia kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za watumishi, iwe ni chachu ya kuwafanya watumishi waweze kutulia katika maeneo yao ya kazi na isiwe chanzo cha uhamisho kwa sababu ya nyumba.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi wa afya ngazi ya kata katika Jimbo la Nanyumbu?
Supplementary Question 2
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Masama kina nyumba kadhaa za watumishi, lakini zimekuwa chakavu sana. Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati nyumba hizi za watumishi ili ziweze kutumika?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwamba tayari tuna mpango pale TAMISEMI Wizarani kwa ajili ya ukarabati wa nyumba chakavu za watumishi ili ziweze kuendana na ubora na hali ya kisasa. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mafuwe kwamba katika vipaumbele, na nyumba hizi chakavu zipo katika kipaumbele chetu na tutaweza kuzirekebisha.
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi wa afya ngazi ya kata katika Jimbo la Nanyumbu?
Supplementary Question 3
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amethibitisha kwamba kukosekana kwa makazi katika baadhi ya maeneo kumesababisha watumishi kuhama na kutokutulia kwenye maeneo hayo, je, Serikali iko tayari kuweka kipaumbele katika maeneo ya vijijini, maeneo ya pembeni katika ujenzi wa nyumba hizo za watumishi ili kuweka utulivu huko?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, hakika kwenye tathmini ambayo tuliifanya kama Wizara, hizi nyumba 2,000 tunazielekeza hasa maeneo ya pembezoni yenye uhitaji mkubwa zaidi ambapo unakuta tumejenga kituo chetu cha afya, lakini hata nyumba za kupanga watumishi hazipo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutaelekeza katika maeneo hayo zaidi ili kuweza kuwa-hold watumishi wetu na waweze kutumikia jamii yetu kule vijijini na maeneo ya pembezoni zaidi.
Name
Dr. Yahaya Esmail Nawanda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za watumishi wa afya ngazi ya kata katika Jimbo la Nanyumbu?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. YAHYA E. NAWANDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Vituo vipya vya Afya vya Mkwedu, Malatu pamoja na Nandwahi hakuna kabisa nyumba za watumishi. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha vituo hivyo vinapata nyumba?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Spika, Serikali inakiri ongezeko la vituo vipya vya afya na zahanati, kwa hiyo kuna upungufu wa nyumba hizo. Tutaelekeza kwenye hizi nyumba 2,000 za three in one angalau ziweze kufikia katika yale maeneo ambayo tumejenga vituo vipya hasa yale maeneo ya vijijini ili watumishi wetu waweze kupata comfort.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved