Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nassor Said Nassor
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO aliuliza:- Je, Serikali kupitia Wizara ya Muungano na Mazingira inachukua hatua gani za kimkakati za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi?
Supplementary Question 1
MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi ya maswali ya nyongeza. Je, Mheshimiwa Wizara imetenga kiasi gani cha bajeti katika kushughulikia suala hili hasa la tabianchi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana na mimi kwenda katika Jimbo langu la Chake Chake kuziangalia hizo athari za tabianchi?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitenga fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia bajeti za sekta mbalimbali ndani ya Serikali ikiwemo bajeti ya maji kwenye kilimo, kwenye miundobinu, kwenye nishati, kwenye misitu ambayo matokeo yake kwa ujumla yanatufanya tuweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Spika, kwa kule Pemba mwaka 2024/2025 Serikali ilipeleka fedha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kujenga kuta za kuzuia athari za maji zinazotokana na bahari kwenye ufukwe wa Sipwese huko Pemba na mwaka uliofuata 2025/2026, Serikali imepeleka shilingi milioni 392 kukamilisha ujenzi wa ukuta huo.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa ukuta huo umefikia 95% kwenye mwaka huu wa fedha. Kwenye bajeti itakayosomwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, itaeleza kiwango kilichotengwa kwenye eneo hili Jimbo la Chake Chake.
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO aliuliza:- Je, Serikali kupitia Wizara ya Muungano na Mazingira inachukua hatua gani za kimkakati za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi?
Supplementary Question 2
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Bonde la Tibirinzi lililopo Chake Chake Pemba limeathirika na mabadiliko ya tabianchi na maji ya bahari kuingia katika bonde hilo na wakulima kushindwa kuendelea na kilimo, je, nini mkakati wa Serikali kujenga tuta katika shamba hilo? Ahsante.
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali imeshayaainisha maeneo yote ambayo yameathirika kutokana na mabadiliko ya tabianchi kule Pemba. Kama nilivyotangulia kusema kwenye jibu langu la nyongeza, ni kwamba kwenye mwaka huu wa fedha 2026/2027, kwenye bajeti ambayo tutaiwasilisha hapa leo, tumeangalia vizuri na kuyaangazia maeneo yote ya Pemba ambayo yameathirika na tutaanza utekelezaji wake hatua kwa hatua.
Name
Abdul Yussuf Maalim
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Amani
Primary Question
MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO aliuliza:- Je, Serikali kupitia Wizara ya Muungano na Mazingira inachukua hatua gani za kimkakati za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi?
Supplementary Question 3
MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uwekezaji katika suala hili la mabadiliko ya tabianchi?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mikakati mbalimbali ya uwekezaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tunayo mikakati ambayo imejikita katika maridhiano ya Kimataifa ambayo tumeyafanya.
Mheshimiwa Spika, kama Taifa tumeshiriki maridhiano ya Rio de Janeiro yaliyofanyika mwaka 1992. Vivyo hivyo tumeridhia makubaliano ya Tokyo yaliyofanyika mwaka 1997. Pia tumeridhia makubaliano ya Paris yanayofanyika mwaka 2015, tunatekeleza na tumeweka mipango kazi ya kutekeleza maridhiano yote hayo.
Mheshimiwa Spika, siyo hivyo tu, Serikali imeendelea na mpango wa kuhakikisha Watanzania wote wanatumia nishati safi na salama, na kwenye hili la nishati safi na salama, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan dunia imemtambua kama champion wa usimamizi wa nishati safi na salama na mtunzaji wa mazingira namba moja ndani ya Tanzania, ndani ya Afrika na nje ya mipaka ya Afrika.
Mheshimiwa Spika, tafiti zilizokuwa zimefanyika zinaonyesha kwamba kila mwaka Tanzania tunapoteza hekta karibia laki 370 za misitu ambayo inatokana na kukata miti kwa ajili ya matumizi ya mikaa na na uharibifu mwingine unaofanyika.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kukabiliana na uharibifu huu ili tuweze kupunguza athari zinazoweza kutokea za mabadiliko ya tabianchi. Kwa hiyo, tumeendelea na zoezi la upandaji miti na Waziri atakaposimama hapa leo, atataja mkakati kabambe wa upandaji miti ambao tunao kwa nchi nzima.
Name
Emmanuel John Khambay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO aliuliza:- Je, Serikali kupitia Wizara ya Muungano na Mazingira inachukua hatua gani za kimkakati za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi?
Supplementary Question 4
MHE. EMMANUEL J. KHAMBAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kutokana na mabadiliko ya tabianchi, Ziwa Babati limevamiwa na magugu na linaenda kupotea. Nini mpango wa Serikali katika kulinusuru Ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Babati?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali inao mpango endelevu wa kukabiliana na athari za mazingira ambazo zimetokea kwenye maziwa yetu, siyo tu Ziwa Babati, tunalo Ziwa Victoria, Ziwa Jipe pamoja na na maziwa mengine.
Mheshimiwa Spika, kwa Ziwa Babati, cha kwanza ambacho tumeweka mkakati ni kushirikiana na Wizara ya Maji ambao ndio wanaohusika na mabonde pamoja na maji ili kwanza tuweke mipaka kwa maana ya kuweka beacons za mipaka ambazo zitaonyesha ukomo wa eneo la shughuli za kibinadamu.
Mheshimiwa Spika, pili, Serikali itaendelea kuwatafutia wananchi wa maeneo yanayozunguka maziwa shughuli mbadala ambazo hazitaathiri maeneo haya ambayo tunalenga kuyahifadhi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved