Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tamima Haji Abass
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha Mawasiliano ya Simu kwenye Vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 1
MHE. TAMIMA HAJI ABASS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nitoe pongezi zangu kwa Serikali kwa juhudi kubwa inayofanya kuhakikisha mawasiliano yanapatikana, na hasa ninampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumeona juzi tu, tarehe 10 Aprili, 2026 alizindua minara 785 kwa ajili ya mawasiliano nchini. Pongezi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa mawasiliano yanaendelea kuimarika, Serikali ina mpango gani sasa kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo kwa urahisi hasa ukizingatia wafanyabiashara wengi wanatumia mitandao kwa ajili ya kufanya biashara zao wakiwemo wanawake?
Name
Switbert Zacharia Mkama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninamshukuru kwa pongezi kwa Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anayofanya kuhakikisha kwamba nchi hii yote inakuwa na mtandao wa kuaminika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwenye jibu lake kwamba Wizara yetu ina mpango mkakati mkubwa wa miaka mitano ya kuhakikisha kwamba nchi hii yote inakuwa na mtandao wa mawasiliano wa kuaminika na katika hilo, hii itatoa kipaumbele kikubwa kwa makundi maalum yakiwemo akina mama, vijana, wenye ulemavu na watu wengine wote walio katika makundi hayo kama wazee na watu wasiokuwa na uwezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumejipanga kuhakikisha, ndani ya miaka hii mitano, kila mwananchi na kila kundi maalum litakuwa na uso wa furaha katika sekta hii ya mawasiliano.
Name
Martha Festo Mariki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuimarisha Mawasiliano ya Simu kwenye Vijiji vyenye changamoto ya huduma hiyo Mkoa wa Kaskazini Unguja?
Supplementary Question 2
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi. Kipande cha kutoka Inyonga mpaka Mpanda na kutoka Mpanda mpaka Uvinza hakina kabisa mawasiliano na maeneo yao yana wanyama wakali. Upi mkakati wa Serikali wa kutuletea minara ili kuimarisha mawasiliano katika maeneo hayo?
Name
Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya maeneo ya Uvinza tumeyajumuisha katika mradi wetu wa kimkakati wa Awamu ya 11 ambao utajenga minara ya mawasiliano katika maeneo yote ya kimkakati kama vile maeneo ya mpakani, maeneo ya SGR, MGR, Tazara, maeneo ya mbuga za wanyama na baadhi ya maeneo ya Jimbo la Uvinza yatajumuishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge kama atahitaji kuyafahamu hayo maeneo, naomba tuonane baada ya kujibu maswali hapa ili niweze kumpa baadhi ya maeneo. Pia maeneo mengine ambayo yatakuwa hayakujumuishwa katika mradi unaokuja wa Awamu ya 11 tutayaingiza katika Mkakati Maalum wa Wizara wa Miaka Mitano ambao unakusudia kuyafikia maeneo yote ya nchi hii, yenye changamoto za mawasiliano ambayo ninaamini kila Mbunge katika jimbo lake ana eneo lenye changamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamhakikishia kwamba ndani ya miaka hii mitano kuanzia mwaka huu wa 2025 mpaka mwaka 2030 tutakuwa tumeyafikia maeneo yote ya changamoto za mawasiliano ya mitandao, tutazimaliza kwa kiasi kikubwa…
MWENYEKITI: Ahsante, malizia.
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: …na tutakuwa tumekamilisha maeneo hayo yote na maeneo ya mtandao tutakuwa tumehakikisha kwamba nchi nzima hii tumeikamilisha.
MWENYEKITI: Nilikuona Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi.
Ninaona kuna wengi hapa wameomba maswali, sitatoa maswali mengine, ninaomba mzime mic. Muda wetu umeisha. (Makofi)
WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, na ninapongeza kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Ninapenda tu kuongezea maelezo machache kuhusiana na swali la Mheshimiwa Mariki, hasa katika upatikanaji wa mawasiliano katika eneo la Inyonga pamoja na Uvinza. Ninapenda tu kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwa upande wa Inyonga tumeshapeleka minara tisa ya TTCL kupitia mradi wetu wa minara 758.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kwa upande wa Uvinza na kwenyewe tumepeleka minara miwili ya Voda. Hata hivyo, kwa upande wa Katavi katika mradi wetu wa awamu ya 10 ambao tumeusaini Disemba hii tumepeleka minara katika kata mbili, lakini vilevile, kwa upande wa Uvinza tumepeleka katika kata tano minara mitatu. Tunaamini ifikapo Machi, 2027, ile miradi ambayo tumeisaini Disemba, 2025 itakuwa imekamilika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved