Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Othman Maulid Suleiman

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mahonda

Primary Question

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN aliuliza:- Je, ipi mikakati ya Serikali ya kuongeza viwanda nchini ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje?

Supplementary Question 1

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nilikuwa ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhamasisha wananchi kuweza kuzipenda na kuzinunua bidhaa zinazozalishwa Tanzania, nikiwa na maana ya kununua bidhaa za Tanzania kwanza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, je, Serikali haioni haja ya kuanzisha programu hii ya kizalendo kwa umma ili ipate mwamko wa kuzipenda bidhaa zetu na kuzinunua? (Makofi)

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niungane na Mheshimiwa Mbunge kwamba jukumu la kukuza, kuendeleza na kuhamasisha bidhaa zetu za ndani ni jukumu letu Watanzania wote. Wizara ya Viwanda na Biashara chini ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Taasisi ya TanTrade tunaendelea kufanya mradi mkubwa wa branding wa bidhaa ambazo zinatengenezwa Tanzania maarufu kama Made in Tanzania Brand.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, pamoja na hayo kupitia miradi mbalimbali ya uendelezaji wa viwanda, tunaendelea kutoa hamasa kwa Watanzania na mwamko sasa hivi umeendelea kuwa mkubwa hasa kwa viongozi wa Serikali na taasisi binafsi ambao tunaendelea kuona wakivaa ama wakitumia bidhaa za Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ninaomba kutoa rai kwa sisi Wabunge kuendeleza hamasa yaku-promote bidhaa zetu za ndani kwa kuzitumia na kuonesha Watanzania kwamba bidhaa zetu zina ubora, zinakidhi viwango na tunazipenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Imamu Mtumwa Vuai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magomeni

Primary Question

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN aliuliza:- Je, ipi mikakati ya Serikali ya kuongeza viwanda nchini ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje?

Supplementary Question 2

MHE. IMAMU MTUMWA VUAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi. Ni lini Serikali itakuja na mkakati madhubuti wa kulinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani wa bidhaa za bei nafuu kutoka nje?

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nishukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na suala la kulinda viwanda vyetu vya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumeendelea kutengeneza sheria, lakini pia tumeendelea kutengeneza kanuni na kuboresha kanuni mbalimbali, lengo ni kulinda bidhaa za ndani, na pia kuchochea uwekezaji na kuendeleza uzalishaji wa bidhaa zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, tunaweza kuona wiki iliyopita Waziri wa Viwanda na Biashara aliongoza zoezi la kukamata mali ambazo zimezalishwa kinyume na sheria ama zimeingizwa kinyume cha sheria ambazo zimeingizwa sokoni chini ya viwango ama kinyume cha taratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la kufanya hivi, ni kulinda viwanda vyetu vya ndani, kuongeza imani ya walaji, lakini pia kulinda mitaji ya Watanzania. Tutaendelea kufanya hivyo ili kuwavutia wawekezaji wapya, lakini pia kulinda wawekezaji na wazalishaji wa bidhaa za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN aliuliza:- Je, ipi mikakati ya Serikali ya kuongeza viwanda nchini ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje?

Supplementary Question 3

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba viwanda vyetu vinazalisha bidhaa ambazo ni shindani, yaani bidhaa ambazo ni sawasawa na zile za nje au zaidi ya zile bidhaa za nje? (Makofi)

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kuanzisha viwanda vipya na kufufua viwanda ambavyo vinaendelea na uzalishaji katika maeneo mbalimbali, tumeendelea kuvutia wawekezaji, na pia kuhamasisha teknolojia mpya na matumizi ya teknolojia mpya kwa uzalishaji wa bidhaa za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, Wizara ya Elimu na Teknolojia, tumeona imeendesha programu mbalimbali za kuongeza ujuzi wa vijana wetu katika vyuo vyetu vya VETA ili kutumia ujuzi mpya, teknolojia mpya, kupunguza gharama ya uzalishaji, kuwa na bei shindani katika soko, lakini kuwa na viwango ambavyo bidhaa zetu zinaweza zikashindana katika soko, siyo tu kikanda, lakini Kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wadau wengine wakiwemo Wizara ya Elimu, tunaendelea kuboresha ujuzi wa vijana wetu ili wazalishe bidhaa zenye ushindani katika soko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN aliuliza:- Je, ipi mikakati ya Serikali ya kuongeza viwanda nchini ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje?

Supplementary Question 4

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Mogitu iliyopo Wilaya ya Hanang ina malighafi ya kutosha ya kutengeneza simenti inayoweza kudumu kwa zaidi ya miaka 100. Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuambatana na mimi ili kwenda kuona rasilimali hii muhimu kwa nchi yetu? (Makofi)

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaomba kupitia Bunge lako kumwahidi Mheshimiwa Mbunge Asia Halamga kwamba, nipo tayari kuambatana naye katika jimbo lake. Pili, kumhakikishia kwamba, Serikali inaendelea na tathmini ya viwanda vya kimkakati kwa kuangalia malighafi ambazo zinaweza kutumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na kuongeza thamani ya bidhaa zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hilo, Mkoa wa Manyara, hususan Jimbo la Hanang, ni miongoni mwa maeneo ya kimkakati ambayo tunaendelea kuangalia uwepo wa malighafi, hasa za chumvi na simenti, ili kuangalia namna gani tunaweza kuvutia wawekezaji kuwekeza katika bidhaa hizo. Lengo ni kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kujihakikishia soko katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN aliuliza:- Je, ipi mikakati ya Serikali ya kuongeza viwanda nchini ili kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje?

Supplementary Question 5

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa, tathmini na eneo la ujenzi wa kiwanda cha mbolea katika Mkoa wa Tabora tayari limepatikana na mwekezaji yupo, ni lini Serikali itaanza mchakato kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea katika Mkoa wa Tabora? (Makofi)

Name

Dennis Lazaro Londo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mikumi

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunafahamu kwamba kilimo ndiyo uti wa mgongo na kimeajiri wengi. Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Dira ya Maendeleo ya 2020 – 2050 inazungumzia ni jinsi gani tunaenda kutumia kilimo kama mhimili wa kutupeleka kwenye uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika muktadha huo, Mheshimiwa Mbunge ataungana nami kujua changamoto ambayo inatukabili kwenye sekta ya kilimo, hasa kutokana na vita inayoendelea kule Ukraine na pia, kule Mashariki ya Kati ambao ndiyo wazalishaji wakubwa wa mbolea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hii inatupeleka kuona kwamba, sisi kama Serikali, tunatafuta majawabu ya uhakika kuona sekta ya kilimo haiyumbi ili kuhakikisha tunaenda kuanzisha viwanda vya mbolea na kuviimarisha vile vilivyopo, ili kutoa majibu ya uhakika katika suala zima la usambazaji wa mbolea na kuimarisha sekta ya kilimo katika nchi yetu, ambayo ndiyo uti wa mgongo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)