Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omary Marcus Msigwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Madaba

Primary Question

MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali italeta fedha katika Jimbo la Madaba ili kutatua changamoto ya maji katika Vijiji vya Gumbiro, Ngadinda na Lilondo?

Supplementary Question 1

MHE. OMARY M. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Waziri ninatamani kujua ni lini utatembelea Mradi huo wa Maji wa Mtyangimbole, Ngadinda na Gumbiro ambapo miradi hiyo imekamilika na maji yapo kwenye matanki isipokuwa hayajafika kwa wananchi na maji yanamwagika pale? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa ushirikiano mzuri ambao anaendelea kuutoa na ninamshukuru sana kwa kutupa taarifa nzuri za maendeleo ya miradi ndani ya Jimbo lake. Miradi hii imefikia hatua nzuri kabisa mpaka sasa Mradi wa Gumbiro upo 90%. Pia, Mradi wa Ngadinda upo 67%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali tumejipanga, na mpaka sasa hatuna changamoto ya kifedha ndani ya miradi hii, na ndiyo maana upo katika hatua nzuri kabisa ya utekelezaji. Ninamtoa hofu Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutekeleza hii miradi na kupeleka fedha ili iweze kukamilika kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameendelea kuomba. Ninakushukuru sana.

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali italeta fedha katika Jimbo la Madaba ili kutatua changamoto ya maji katika Vijiji vya Gumbiro, Ngadinda na Lilondo?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali moja la nyongeza. Wilaya ya Muleba ni kati ya wilaya kongwe na yenye matatizo makubwa sana ya maji kutokana na jiografia yake. Tuna mradi wa kutoa Maji Ziwa Victoria ambao usanifu umekamilika na ninashukuru Mheshimiwa Rais aliyouongelea wakati wa kampeni; je, ni lini utekelezaji au ujenzi wa mradi huu kwa ajili ya wakazi wa Wilaya ya Muleba utaanza? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Muleba Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kumpongeza sana kwa kazi nzuri sana kwa sababu katika utekelezaji wa miradi ya maji, cha kwanza tunafanya need assessment na Mheshimiwa Mbunge alitoa mchango mkubwa sana katika kubainisha mahitaji ya mradi ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo tulifanya upembuzi yakinifu na baada ya hapo, tukafanya usanifu wa kina. Kinachofuatia ni Serikali kutafuta fedha, na sasa tuko katika michakato mbalimbali ya kuhakikisha kwamba fedha inapatikana ili iweze kwenda kutekeleza mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Serikali hii ambayo imejipambanua kuhakikisha kwamba inamtua mama ndoo kichwani, Wanamuleba wako ndani ya mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba watapata huduma ya majisafi na salama kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameendelea kufuatilia kwa niaba yao. Ninakushukuru sana. (Makofi)

Name

Chief Thomas Mgonto Kitima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ikungi Mashariki

Primary Question

MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali italeta fedha katika Jimbo la Madaba ili kutatua changamoto ya maji katika Vijiji vya Gumbiro, Ngadinda na Lilondo?

Supplementary Question 3

MHE. THOMAS M. KITIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii na mimi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Ikungi Mashariki, kuna visima vingi vilichimbwa, lakini maji hayajaweza kusambazwa katika maeneo mbalimbali. Mfano mzuri ni Kijiji cha Misule, Kata ya Misughaa. Je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuhakikisha kwamba wananchi wale wa Kata ya Misughaa, Kijiji cha Misule wanaweza kusambaziwa maji na wanaweza kupata hayo maji ili waweze kuwa na imani ya Serikali yao kwa maana ya kumtua mama ndoo kichwani?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye upande wa maeneo ya Misughaa, kwanza kabisa Serikali itachimba visima na baada ya kuchimba visima tunafanya pump test na baadaye tunajiridhisha na que ya maji. Tukishajiridhisha na que ya maji, maana yake sasa ndiyo tunafanya usanifu wa kutengeneza mtandao unaoendana na maji ambayo yanazalishwa pale. Kwa hiyo, tukishajiridhisha, baadaye sasa tunayafikisha kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bajeti ya kwanza ilikuwa kuchimba visima, bajeti ya pili ni kusambaza baada ya kujiridhisha na uwingi wa maji yaliyopatikana katika visima. Ninamtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwa vile tumekamilisha uchimbaji wa visima na pump testing imeishafanyika. Sasa tuko kwenye mchakato wa kuingiza katika bajeti ya kuhakikisha kwamba sasa tunaenda kujenga mtandao wa maji ili maji yawafikie watumiaji na wananchi wa Misughaa. Ninakushukuru sana.

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. OMARY M. MSIGWA aliuliza: - Je, lini Serikali italeta fedha katika Jimbo la Madaba ili kutatua changamoto ya maji katika Vijiji vya Gumbiro, Ngadinda na Lilondo?

Supplementary Question 4

MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Mradi wa Maji wa Mazimbu uliopo Kata ya Matwiga ambao utekelezaji umekwenda 65% pamoja na mradi wa Maji wa Kambikatoto ambao utekelezaji wake upo zaidi ya 90% umesimama kwa sasa hivi na wakandarasi wameshaondoka site, je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha ili miradi hii ya maji iweze kutekelezwa na wananchi waweze kunufaika kama lengo lilivyokusudiwa? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi unapofikia 90%, maana yake umekaribia kutoa huduma ya maji kwa wananchi. Tunayo maelekezo ya Mheshimiwa Waziri, na mimi nimepewa maelekezo ya kusimamia miradi yote ambayo iko ukingoni kutoa huduma kwa wananchi, ni bora ikakamilika ili wananchi waweze kupata matokeo katika miradi hiyo huku tukiwa tunaendelea na miradi mingine ambayo iko katika hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu Mjumbe wetu wa Kamati yetu ya Maji na Mazingira kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye Jimbo la Lupa la kuwasemea wananchi ikiwemo hata ule Mradi wa Miji 28 ambao upo katika hatua mbalimbali za mazungumzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuhakikishia Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kwenda kuhakikisha kwamba miradi ya aina hiyo inakamilika na kutoa matokeo kwa wananchi wakiwemo wananchi wa Lupa. Ninakushukuru sana.