Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Japhael Masanja Lufungija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA Wilaya ya kaliua ili kufungua barabara katika vijiji vipya 22 vilivyopo Jimbo la ulyankulu?

Supplementary Question 1

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, ninaanza kwa kupongeza kwa juhudi kubwa za namna ambavyo Serikali inaendelea kuongeza mtandao na fedha kwenye barabara zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza. Kwa kuwa barabara ya Chemba – Nhw’ande – Twigu inayounganisha Kata ya Sasu ni barabara ndefu sana ukilinganisha na fedha zilizotengwa. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba sasa zinajengwa karavati ili barabara iweze kupitika kwa wakati wote?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Barabara ya King’wangoko – Usonga imepewa fedha shilingi milioni 416; lakini barabara hiyo inapitika kwa kipindi cha kiangazi tu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inajenga daraja pale Mto Igombe? Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuambatana na mimi baada ya Bunge kwenda kutembelea barabara hizo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Japhael Masanja Lufungija amefuatilia sana ujenzi wa barabara katika Jimbo la Ulyankulu. Nimhakikishie kwamba Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha kuwa barabara za vijijini na mijini zinajengwa na zinapitika vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, barabara hizo ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja, zote mbili nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea kwanza na tathmini ya mahitaji ya fedha kufuatia uharibifu wa mvua nyingi zilizoonyesha pote nchini, ikiwemo katika Jimbo la Ulyankulu; na tutapeleka fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kumwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Kaliua kuhakikisha kwamba wanafanya tathmini na kuwasilisha ongezeko la mahitaji ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo. (Makofi)

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA Wilaya ya kaliua ili kufungua barabara katika vijiji vipya 22 vilivyopo Jimbo la ulyankulu?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itapeleka fedha ya kujenga barabara ya Kisiwani kwa Fufana iliyopo katika Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Chaurembo kwamba tunafahamu katika Jimbo la Mbagala katika Manispaa ya Temeke kama ilivyo kote nchini, eneo la Chamazi tunahitaji kujenga barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mipango kadhaa. Moja, mpango wa kawaida wa bajeti ya mwaka huu wa fedha 2025/2026 ambapo tunaendelea na utekelezaji. Tumefanya tathmini ya mahitaji ya fedha za dharura kwa ajili ya barabara zilizoharibiwa na mvua, ambapo tunahitaji takribani shilingi bilioni 120. Serikali iko kwenye taratibu za kupata fedha hizo kwa ajili ya kujenga barabara hizo. Nimhakikishie Mheshimiwa Chaurembo kwamba barabara hizo zitapewa kipaumbele.

Name

Sara Msafiri Ally

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA Wilaya ya kaliua ili kufungua barabara katika vijiji vipya 22 vilivyopo Jimbo la ulyankulu?

Supplementary Question 3

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini TARURA itatenga fedha kwa ajili ya kujenga barabara za kiwango cha zege kwenye maeneo ya milimani kama ilivyo Wilaya ya Mvomero ambapo maeneo mengi yako milimani na barabara zinaharibika kipindi cha mvua?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sara Msafiri, Mbunge wa Mvomero amefuatilia mara kadhaa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kuhusu suala la barabara za Mvomero. Ni kweli, wote ni mashuhuda kwamba Mvomero imekuwa na mafuriko mengi sana na ya mara kwa mara, ikiwemo mwaka 2026. Matokeo yake barabara zetu nyingi za udongo zinazolewa na maji na tunakuwa tunaanza upya mara kwa mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI tuko kwenye hatua za mwisho za kufanya design ya barabara madhubuti na imara zaidi ambazo zitajengwa kwenye maeneo yenye mafuriko, milima na mvua nyingi zaidi ili tuhakikishe kwamba barabara hizo zinadumu na zinahudumia wananchi kwa muda mrefu zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumhakikishie Mheshimiwa Sara Msafiri na wananchi wa Mvomero kuwa Serikali sikivu iko kwenye hatua za utekelezaji na tutahakikisha kwamba tunaboresha barabara hizo.

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA Wilaya ya kaliua ili kufungua barabara katika vijiji vipya 22 vilivyopo Jimbo la ulyankulu?

Supplementary Question 4

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Wilaya ya Kakonko ina mtandao wa barabara wa kilometa 391.24 na uwezo wa TARURA ni kufanya matengenezo kilometa 120 tu sawa na 30.6%. Je, ni lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA katika Wilaya ya Kakonko?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba bajeti ya TARURA kila mwaka, kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 imeendelea kuongezeka. Kwa mfano, kutoka shilingi bilioni 210 mwaka 2021/2022 mpaka mwaka huu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 870, ukiondoa fedha za dharura.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunatambua kwamba uhitaji wa fedha ni mkubwa zaidi, lakini tutaendelea kutenga fedha kwa awamu kujenga barabara za Kakonko ili wananchi waweze kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Name

Moshi Selemani Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya TARURA Wilaya ya kaliua ili kufungua barabara katika vijiji vipya 22 vilivyopo Jimbo la ulyankulu?

Supplementary Question 5

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mvua zilizonyesha zimeharibu barabara nyingi kwenye eneo la Wilaya ya Tanganyika, ikiwemo Barabara ya kutoka Kapanga – Bujombe – Kalia, je, ni lini Serikali itakwenda kufanya ukarabati kwa barabara nyingi zilizoharibika kwenye eneo la Wilaya ya Tanganyika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba katika jimbo la Tanganyika, kama ambavyo ipo katika majimbo takribani yote kote nchini, kumekuwa na uharibifu mkubwa wa barabara zetu za TARURA. Serikali imeshafanya tathmini ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo linafanyika sasa, kwanza maeneo mengi bado mvua zinaendelea kunyesha kwa hivyo, siyo rahisi kufanya matengenezo ya uhakika katika kipindi hiki cha mvua. Tunasubiri kwanza hali ya hewa ikae vizuri, mvua zipungue, na baada ya hapo, taratibu za fedha zinaendelea kufanyika ili tuendelee kujenga barabara hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kakoso kwamba suala hilo liko kwenye pipeline na tutakwenda kuhakikisha kwamba tunajenga barabara hizo.