Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri ninaomba niulize maswali madogo mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mtandika - Ikula kilometa 18 katika Kata ya Ruaha Mbuyuni hii barabara haipitiki. Ni lini sasa itakarabatiwa ili iweze kupitika hata pikipiki ziweze kupita? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Ndengisivili - Kimala pia ipo katika Kata ya Kimala ni lini itakarabatiwa? Kwa sababu kuna maeneo tu machache ambayo yamekuwa korofi hayapitiki wakati wote wa mvua. Je, lini sasa Serikali itaangalia maeneo ambayo korofi yaweze kukarabatiwa ili barabara ziweze kupitika kwa mwaka mzima? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli zipo baadhi ya barabara ambazo zimeathirika na mvua na mafuriko, lakini pia zipo barabara ambazo hazijafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara kwa muda mrefu na Serikali imekwishazitambua barabara hizo zote zikiwemo barabara za Wilaya ya Kilolo barabara ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja Mtandika - Ikula ya kilometa 18 na Ndengisivili - Kimala ambazo hazipitiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie nafasi hii kwanza nimkumbushe na kumwelekeza Meneja wa TARURA wa Mkoa Iringa na wa Wilaya ya Kilolo kuhakikisha kwamba wanazifanyia tathmini haraka barabara hizi na kujua gharama inayohitajika ili waweze kuleta maombi hayo Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa ajili ya ukarabati ili angalau ziweze kupitika vizuri, ahsante. (Makofi)

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Tima - Mapemba - Oysterbay hadi Kwa Mapunda umeshasainiwa. Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo kulingana na mkataba utaanza?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafanya taratibu baada ya kusaini mikataba kuna taratibu ambazo wakandarasi wanafanya zikiwemo mobilization, lakini pia mara nyingine advance payment. Kwa hiyo, nikuhakikishie tu barabara hii ambayo umeitaja Mbunge wa Mbagala, Mheshimiwa Chaurembo, tumesaini maktaba kama ulivyosema hatua zinazofuata sisi Serikali tutaisukuma kwa haraka zaidi ili mkandarasi aanze ujenzi mapema iwezekanavyo ili wananchi waweze kunufaika na mpango huo mzuri wa Serikali. (Makofi)

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 3

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi, Barabara ya Liwale - Nahoro, Liwale – Mpigamiti, Liwale – Ndapata, Liwale - Kikulyungu ni barabara zilizoharibika sana na mvua hizi zinazoendelea. Nini mpango wa Serikali kuzifanyia ukarabati barabara hizi? (Makofi)

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya Majimbo ambayo yamepata kipaumbele cha bajeti ya fedha za TARURA ni pamoja na Jimbo la Liwale kutokana na kuathirika kwa kiasi kikubwa na mvua, lakini barabara zake nyingi zilikuwa zimeharibika kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara hizo tunazitambua na tumeziweka kwenye mpango kwa ajili ya ukarabati kwa awamu. Niwahakikishie wananchi wa Jimbo la Liwale kwamba Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kupeleka fedha kwa awamu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba barabara hizo zinapitika vizuri. (Makofi)

Name

Kasalali Emmanuel Mageni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 4

MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, mwaka 2022/2023 Serikali ilipeleka pesa kwa ajili ya kujenga Barabara ya kutokea Ilumba – Mwakaluto - Goloma ambayo ilikuwa ni muhimu sana kwa ajili ya kupitisha mazao, lakini barabara hii kwa sasa kutokana na mvua imesombwa yote haipitiki.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kupeleka pesa ya dharura ili barabara hii muhimu kwa Jimbo ya Sumve iweze kujengwa upya? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaona umuhimu wa kupeleka fedha kwenye barabara hiyo katika Jimbo la Sumve, Wilaya ya Kwimba na nitumie nafasi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA Wilaya Kwimba na Mkoa wa Mwanza kuifanyia tathmini barabara hiyo, kujua gharama zinazohitajika kwa ajili ya matengenezo maeneo korofi ili Ofisi ya Rais, TAMISEMI iweze kupeleka fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba barabara hizo zinafanyiwa matengenezo na zinaanza kupitika vizuri zaidi. (Makofi)

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 5

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mvua zinazoendelea kunyesha katika Jimbo la Hai zimefanya uharibifu mkubwa wa barabara; Barabara ya Mferejini - Kwa Tito – Boma - Kikavu Chini pale Kisereni, Kwa Mengi kwenda Kiria - Somali kwenda Tindigani, Tindigani kwenda Rundugai lakini pia Barabara ya Makoa Mferejini eneo la Kwa Mengi pale na barabara nyingine nyingi hazipitiki kwa sasa.

Je, Serikali ina mpango wa haraka wa kufanya ukarabati barabara hizi ili ziweze kupitika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba mvua ambazo zimeendelea kunyesha kote nchini zimekuwa na madhara mbalimbali kwenye barabara zikiwemo barabara za Jimbo la Hai na nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara hizo zote ambazo amezitaja kwa bahati nzuri ameshazileta kwa maandishi Ofisi ya Rais, TAMISEMI na sisi tumeshaweka kwenye mpango kwa awamu kwa ajili ya kuzikarabati ziweze kupitika.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Hai kwamba Serikali itazifanyia kazi barabara hizo ili ziweze kupitika vizuri, ahsante. (Makofi)

Name

Aziza Sleyum Ally

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 6

MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Kwa kuwa barabara hizi zinasimamiwa na TARURA. Serikali imeongezea kiwango kikubwa cha pesa TARURA, lakini bado barabara zina shida za kuweza kupitika. Je, Serikali ina mpango gani wa kuangalia Mfuko huu wa TARURA ili barabara hizi ziweze kupitika kwa muda mrefu zaidi kuliko sasa pesa zinakwenda, lakini bado barabara zinakuwa mbovu? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, niseme jambo moja muhimu kwamba katika kipindi hiki cha miaka minne Serikali imeongeza sana mtandao wa barabara za TARURA. Kwa hiyo, barabara nyingi mpya zimeendelea kufunguliwa na kujengwa na hiyo imepelekea mahitaji ya fedha za barabara kuendelea kuongezeka na Serikali imeongeza bajeti ya barabara kutoka shilingi bilioni 275 mwaka wa fedha 2021/2022 mpaka shilingi bilioni 870.3 mwaka wa fedha 2024/2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ambayo Bunge hili Tukufu imepitisha wiki mbili zilizopita Mheshimiwa Rais ameongeza tena bajeti ya TARURA kutoka shilingi bilioni 870.3 mpaka shilingi trilioni 1.130. Kwa hiyo, jitihada za Serikali zipo wazi za kuongeza fedha na uwezo wa TARURA na niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba barabara hizo zinazoathirika zitaendelea kujengwa kwa awamu. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 7

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, kwanza, ninaishukuru sana Serikali kupeleka fedha shilingi milioni 400 kujenga Daraja la Mto Tigite kuunganisha pale Matongo. Kuna ahadi ya Mawaziri wa TAMISEMI wawili waliopita kutoa kilometa moja ya lami Sirari - Nyamongo na Halmashauri ya Nyamwaga Makao Makuu.

Je, ni lini ahadi hiyo ya Serikali itatekelezwa katika maeneo yale pale, ukizingatia kwamba Tarime ni Jimbo la Kanda Maalum na mambo yake ni maalumu sana? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI alifanya ziara katika Jimbo la Tarime Vijijini na akatoa ahadi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kilometa moja katika eneo hilo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na Wananchi wa Jimbo la Tarime Vijijini kwamba Serikali ikiahidi inatekeleza na sisi sote ni mashahidi kwamba ahadi zote ambazo Serikali imekuwa ikitoa imekuwa ikitekeleza. Kwa hiyo, wananchi wawe na amani, Serikali ipo kwenye hatua nzuri za kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza kujenga barabara hiyo kwa awamu ili iweze kuwa kiwango cha lami. (Makofi)

Name

Mary Pius Chatanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 8

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi; ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya barabara ambazo zipo Jimbo la Newala Vijijini zisizopitika hasa Mkoma II kwenda Chimemena lakini pia ile ya Malatu Shuleni - Mchauru hadi Mpalu ili ziweze kupitika kwa urahisi? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaje hiyo ya Mkoma II kwenda Chimemena na nyingine zote ni moja ya barabara ambazo Ofisi ya Rais, TAMISEMI kupitia TARURA inazitambua, imeziainisha na inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kwenda kuzitengeneza ili ziweze kupitika vizuri.

Kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mtanda na Wananchi wa Jimbo la Newala Vijijini kwa Serikali tayari imezitambua na tayari inatenga bajeti kwa awamu na barabara hizo zitatengenezwa ili ziweze kupitika vizuri zaidi.

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 9

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara nyingi za Mkoa wa Simiyu zile za ndani zote zimekatika na wakulima wanapata shida sana kusafirisha mazao kutoka shambani kupeleka nyumbani, vivyo hivyo na wafanyabiashara ni tatizo kubwa. Je, ni lini Serikali itakarabati barabara hizo ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu wafanye kazi kwa ufanisi? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya mikoa ambayo imepata kipaumbele kikubwa cha fedha za barabara kwa ajili ya ukarabati barabara za vijijini na mijini ni Mkoa wa Simiyu na nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa tunapoongea Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika Mkoa wa Simiyu wanaendelea na ukarabati wa barabara makalvati na madaraja katika maeneo mbalimbali na hizo barabara ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja nimhakikishie tu kwamba Serikali itazifikia kwa ajili ya kuzikarabati na kuhakikisha kwamba zinapitika vizuri. (Makofi)

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha barabara za mitaani zinafanyiwa ukarabati na maboresho ili kuepusha usumbufu wakati wa mvua?

Supplementary Question 10

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi; Mji wa Bunda unakua, lakini cha ajabu barabara ya lami ipo moja tu kutoka pale kwenda Bomani na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya alituahidi kutujengea barabara ya lami kilometa moja, moja katika Mitaa ya Bunda. Ni lini sasa mtatujengea barabara ya lami kwenye Mitaa ya Bunda ili iendane na hadhi ya Mji wa Bunda? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mji wa Bunda unakuwa kwa kasi na Mheshimiwa Mbunge mara kwa mara amekuwa akiwasemea pia wananchi wa eneo la Bunda kwa ajili ya kuona miundombinu inakuwa vizuri na mimi ninaomba nikuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini, kwamba Serikali inatambua uhitaji wa barabara za lami na ahadi za viongozi wetu wa kitaifa ni kipaumbele na tutakwenda kutekeleza ujenzi wa barabara hizo kwa awamu.

Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Ester Bulaya na Wananchi wa Bunda Mjini kwamba Serikali hii sikivu itakwenda kujenga barabara hizo kwa awamu. (Makofi)