Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 60 | 2026-04-10 |
Name
Stella Ikupa Alex
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Wagonjwa wenye Ulemavu wa Akili wanapata Dawa bure kwa kuwa siyo wote wana Bima ya Afya?
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inayoelekeza kutoa huduma za msamaha wa gharama za matibabu kwa watu wasio na uwezo na wenye magonjwa sugu kama saratani, UKIMWI, kisukari pamoja na wagonjwa ya akili.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeshatangaza rasmi kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote awamu ya kwanza, itakayohusisha makundi ya wananchi ikiwa ni pamoja na watoto, wajawazito, walemavu na wengine wasio na uwezo, ambapo kundi hili litagharamiwa na Serikali. Kukamilika kwa hatua hii kutawawezesha wananchi, wakiwemo walemavu wenye tatizo la afya ya akili kupata huduma pasipo kuwa na kikwazo cha fedha.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved