Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 28 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 356 2025-05-20

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta muswada wa sheria kuwalinda watoto wa kike wanaofanyiwa vitendo vya usagaji nchini?

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai, 2023 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokea taarifa ya Tume ya Kuangalia namna ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai ambapo miongoni mwa mapendekezo ilikuwa ni kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali za haki jinai ikiwemo Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume na hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Haki Jinai (The Criminal Justice (Miscellaneous Amendment) Bill) ambapo kifungu cha 176 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kimependekezwa kufanyiwa marekebisho ili kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo vitendo vya usagaji kwa watoto wa kike.