Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 10 Other Sectors Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 105 2026-04-16

Name

Dougras Didas Massaburi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kivule

Primary Question

MHE. DOUGRAS D. MASSABURI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Msongola – Mbande hadi Chamazi kwa kiwango cha lami?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dougras Didas Massaburi, Mbunge wa Kivule, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Msongola – Mbande (kilometa 7.4) ni sehemu ya Barabara ya Chanika – Mbagala Rangitatu yenye jumla ya kilometa 29.2 ambapo jumla ya kilometa 25.4 zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, ujenzi wa kilometa 3.8 zilizobaki katika sehemu ya Msongola – Mbande unaendelea ambapo kwa sasa jumla ya kilometa 1.6 zimewekwa tabaka la lami, kilometa 1.1 zipo kwenye tabaka la kokoto (CRR) na kilometa 1.1 zipo kwenye hatua za matabaka ya udongo. Ujenzi wa barabara hii unatarajia ukamilike mwezi Juni, 2026.