Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 128 2026-04-20

Name

Sheila Edward Lukuba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga mfereji mkubwa kuelekeza maji Mto Ngerengere ili kunusuru wakazi wa Kata ya Kihonda na Lukobe kwa mafuriko?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Sheila Edward Lukuba, Mbunge wa Viti Maalumu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Kihonda na Lukobe katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro zimekuwa zikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati za mvua. Ili kutatua changamoto hiyo, Serikali imepanga kujenga mifereji ili kuyaelekeza maji katika Mto Ngerengere. Serikali imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathimini na kuandaa andiko la mradi ambalo litaonesha mahitaji halisi na njia nzuri ya kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, timu ya tathimini inatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla au ifikapo Septemba 2026. Ahsante.