Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 49 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 634 | 2025-06-19 |
Name
Dr. Jasson Samson Rweikiza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:-
Je, lini Kilimo cha Mazao ya Alizeti na chikichi kitaanza Mkoani Kagera kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais akiwa Bukoba Juni, 2022?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika jitihada za kukuza kilimo cha mazao ya alizeti na chikichi katika Mkoa wa Kagera, Serikali kati ya mwaka 2021 na 2025 imesambaza jumla ya miche ya michikichi 15,840 katika Mkoa wa Kagera ili kuimarisha uzalishaji wa zao hilo. Pia, miche ya chikichi 2,908 inaendelea kutunzwa katika vitalu vya TARI - Maruku kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima wa zao la chikichi katika Mkoa wa Kagera.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali imehamasisha wakulima katika Mkoa wa Kagera kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti kutoka tani 2,716.64 mwaka 2023 hadi tani 3,047 mwaka 2024, sawa na ongezeko la 12.16%.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved