Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 49 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 629 2025-06-19

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: -

Je, zipi sababu za kuwa na gharama tofauti ya kuingiza Umeme majumbani Kibaha Vijijini badala ya kuwa na bei moja ya shilingi 27,000.00 tu?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetofautisha gharama za kuunganisha umeme kulingana na eneo husika ambapo kwa maeneo ya vijijini, gharama za kuunganisha umeme ni shilingi 27,000.00 na kwa maeneo ya mijini yakiwemo maeneo ya Miji Midogo gharama ni shilingi 320,960.00.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa eneo la Kibaha Vijijini, Kata za Kwala na Dutumi ni maeneo yanayopakana, vijijini hivyo vinalipa shilingi 27,000.00 kama gharama ya kuunganisha umeme. Aidha, maeneo yanayopatikana katika Kata za Mlandizi, Mtongani, Kawawa, Janga, Kikongo, Kilangalanga, Boko na Soga ni maeneo ya Mji Mdogo, hivyo wateja wa maeneo hayo wanalipia shilingi 320,960.00 kama gharama ya kuunganisha umeme.