Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Finance Wizara ya Fedha 528 2025-06-06

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -

Je, Serikali imepoteza fedha kiasi gani mwaka 2015 - 2020 kwa kutokuwepo usalama madhubuti wa mifumo ya usimamizi kufuatia mabadiliko ya TEHAMA? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mabadiliko ya TEHAMA yametumika kama fursa ya kujenga mifumo yetu wenyewe ya kukusanya mapato na kudhibiti matumizi. Mifumo hiyo imeiwezesha Serikali kukusanya mapato kwa ufanisi na hivyo kudhibiti kiwango cha uvujaji wa mapato kilichokuwepo kutokana na kutotumia mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato. Kwa mfano, mara baada ya kuanza kutumia mfumo wa kukusanya mapato wa GePG, mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na Wizara, idara na taasisi yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 689 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi trilioni 2.21 mwaka 2019/2020 ikiwa ni ongezeko la takriban 400%.