Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | 481 | 2025-06-02 |
Name
Stella Ikupa Alex
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. STELLA I. ALEX aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani wa kuifanya lugha ya alama kuwa lugha rasmi ya mawasiliano?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua lugha ya alama kama mojawapo ya lugha rasmi za mawasiliano miongoni mwa wenzetu wenye changamoto ya usikivu hafifu. Aidha, Kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) za mwaka 2019, Kifungu cha 34 (1 - 3) na 35 (1 - 3) vinaeleza namna bora ya usimamizi na uendeshaji wa ukalimani wa lugha ya alama ikiwa ni pamoja na kuunda kanzidata ya wakalimani wa lugha hiyo na kuratibu utumiaji wao katika shughuli mbalimbali za kiserikali na kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kusaidia ukuaji na weledi katika taaluma hii kwa kuwapatia mafunzo ya msasa yatakayowasaidia kuwa wakalimani bora na wanaoweza kutumiwa ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali kadhalika, kupitia Kanuni hizo, tayari kanzidata ya wakalimani wa lugha hiyo imeanza kuundwa ambapo zaidi ya wakalimani 300 wamejisajili na hatua inayofuata ni kuwapa mafunzo na kubainisha wale wanaokidhi vigezo. Vilevile, muundo wa utumishi wa kada hii tayari umeandaliwa. Hatua nyingine zilizopangwa na Serikali ni pamoja na kuwawezesha wale watakaokidhi vigezo kujifunza pia alama za Kimataifa ili waweze kutumiwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved