Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 579 | 2025-06-12 |
Name
Vincent Paul Mbogo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Bwawa la Lambo la kunyweshea mifugo Kijiji cha Kacheche na ujenzi wa Josho Nyikankulu, Kata ya Chala, Nkasi Kusini?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Nkasi Kusini, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imejenga Bwawa la Kacheche kupitia Mpango wa Kuendeleza Kilimo (ASDP I) kati ya Mwaka 2008 na 2009. Hata hivyo kwa kuwa, bwawa hilo limejengwa muda mrefu, kwa sasa limejaa tope, na hivyo kupunguza uwezo wake wa kuhifadhi maji. Kutokana na hali hiyo, Serikali itatuma timu ya wataalam kufanya tathmini ya hali halisi ya bwawa hilo, ili hatua stahiki za kukamilisha ujenzi huo ziweze kuchukuliwa.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na ujenzi wa majosho katika maeneo mbalimbali hapa nchini, likiwemo Josho la Nyikankulu lililopo Kata ya Chala, Nkasi Kusini, kadiri ya upatikanaji wa fedha. Aidha, Naomba kutoa rai kwa Halmashauri ya Nkasi kutenga fedha kutoka kwenye mapato yake ya ndani, kwa ajili ya kujenga majosho katika maeneo yenye uhitaji wa huduma hiyo Wilayani Nkasi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved