Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 428 | 2025-05-27 |
Name
Dr. Paulina Daniel Nahato
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha huduma ya TEHAMA maeneo wanayotumia Wanafunzi kujisomea katika Vyuo Vikuu vya Umma?
Name
Omari Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inafanya maboresho ya Miundombinu ya Internet; Mifumo ya Kujifunzia Kidijitali (LMS); Maktaba za Kidijitali; Elimu kwa Studio za Multimedia; Mifumo ya Kiutawala Kidijiti na kununua Vifaa kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum katika Vyuo Vikuu vya Umma. Lengo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa elimu ya juu wanapata mazingira bora ya kujisomea yanayochochea ujifunzaji wa kisasa, jumuishi, na unaotumia teknolojia kwa tija.
Mheshimiwa Naibu Spika, mafanikio ya maboresho haya ni hatua muhimu katika mwelekeo wa kuifanya elimu ya juu nchini kuwa ya kisasa, jumuishi na yenye ushindani wa Kimataifa ili kufikia ajenda ya mageuzi ya elimu ya juu hapa nchini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved