Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 32 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 402 2025-05-26

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka Watumishi katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga ili kupunguza changamoto iliyopo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya watumishi wa kada ya afya 34,720 wameajiriwa na kupangiwa vituo kote nchi. Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2024/2025 Halmashauri ya Mji wa Mbinga imepokea jumla ya watumishi 102 wa kada za afya na watumishi 36 wamepangiwa hospitali za wilaya na 66 katika vituo vya afya na zahanati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya kwa awamu na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu wa wataalam, ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Mbinga.