Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 32 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 402 | 2025-05-26 |
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga Nyumba za Walimu kufuatia ujenzi wa Shule nyingi nchini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2024/2025 Serikali imetoa shilingi bilioni 13.79, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 263 (one in one) katika shule za msingi nchini. Vilevile, shilingi bilioni 14.82 imepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya nyumba za walimu 741. Aidha, mwaka 2025/26 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 54 (two in one).
Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha za kujenga na kufanya ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa kutoa kipaumbele kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved