Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 697 2025-06-26

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaongeza wataalam wa afya katika Hospitali ya Bugando na Sekou Toure kwa kuwa kuna upungufu mkubwa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Juni, 2025 Serikali imeajiri watumishi wapya 175 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na watumishi 79 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure hivyo kuendelea kupunguza upungufu uliopo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa kibali cha ajira za watumishi wa kada mbalimbali 144 kwa Hospitali ya Kanda Bugando ambapo taratibu za ajira zinaendelea.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)