Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 54 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 696 | 2025-06-26 |
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Laela – Mwimbi – Kizombwe (Matai) yenye urefu wa kilometa 92 yameanza ambapo zabuni kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na uandaaji wa nyaraka za zabuni ipo katika hatua ya kufanyiwa upekuzi (vetting).
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zinatarajiwa kuchukua kipindi cha mwaka mmoja baada ya mkataba kusainiwa. Usanifu utakapokamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved