Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 695 2025-06-26

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuunganisha barabara kutoka Nyamilangano – Ushetu hadi Kaliua Tabora?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Nyamilangano – Ushetu – Kaliua ni sehemu ya barabara ya Mpanda – Ugalla – Kaliua – Ulyankulu – Kahama yenye urefu wa kilometa 457. Kazi ya upembuzi yakinifu (feasibility study) wa barabara hiyo imekamilika na mkataba wa kumpata mhandisi mshauri kwa ajili ya usanifu wa kina umewasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya upekuzi (vetting). Kazi ya usanifu wa kina itachukua muda wa miezi 12. Baada ya usanifu wa kina kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.