Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 54 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 694 | 2025-06-26 |
Name
Tarimba Gulam Abbas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kinondoni
Primary Question
MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza:-
Je, Serikali haioni haja ya kutafuta fedha kama mikopo kuliko kutegemea Bajeti ya Serikali katika kuweka lami, taa na mifereji barabara za ndani Dar es Salaam?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara za ndani katika Jiji la Dar es Salaam, na kwa kutambua ufinyu wa bajeti ya ndani, Serikali imechukua hatua za makusudi za kutafuta vyanzo mbadala vya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya miji.
Mheshimiwa Spika, moja ya hatua ambazo Serikali imechukua ni utekelezaji wa Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) unaofadhiliwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Mradi huu unalenga kuboresha barabara za ndani, mifereji ya maji ya mvua, taa za barabarani na maeneo ya wazi.
Mheshimiwa Spika, katika Manispaa ya Kinondoni kilometa 58.14 zitajengwa kwa kiwango cha lami, pamoja na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, njia za watembea kwa miguu, taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua na kupandwa kwa miti pembezoni mwa barabara ili kuimarisha mazingira. Mradi umekwishaanza na utekelezaji unaendelea. Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha kuwa miundombinu ya miji inaboreshwa ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi, usalama na ustawi wa wananchi wake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved