Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 693 2025-06-26

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga bweni la wasichana na wavulana katika Shule ya Sekondari ya Kimaiga, Kata ya Kihanga?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa shule kuwa na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo uwepo wa mabweni. Hata hivyo, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni ujenzi wa shule mpya za kutwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi na watoto kutembea mwendo mrefu na kuongeza nafasi katika shule za kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2020/2021 - 2024/2025 Serikali imetumia shilingi bilioni 1.94 kujenga shule mbili za kata na mabweni sita katika Shule za Mgama, Kiponzelo na Weru kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za ujenzi wa miundombuni ya elimu kadri ya upatikanaji wa fedha.