Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 692 2025-06-26

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha uwezo wa kibajeti na rasilimali watu kwa TARURA ili kuwezesha ujenzi wa barabara za kudumu zenye viwango bora zaidi. Lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora ya usafiri wakati wote wa mwaka na pia kuhakikisha barabara zinajengwa kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya kudumu na kwa kufuata usanifu wa kina uliofanyika huku ukizingatia viwango vya ubora vilivyowekwa, hususani katika kukabiliana na athari za hali ya hewa hasa katika nyakati za mvua.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa barabara nyingi za vijijini bado ni za udongo na changarawe. Barabara hizi ni rahisi kuathiriwa na mvua nyingi na magari makubwa yanayozidi uwezo wake wa kubeba mizigo. Hali hii husababisha barabara hizi kuharibika haraka kuliko muda uliokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na mijini kwa kuzijenga katika viwango vya kudumu kulingana na upatikanaji wa fedha.