Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 54 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 690 2025-06-26

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha majengo ya Mradi wa Dege Beach-NSSF Mbweni kwa kuwa ni wa muda mrefu?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya tathmini ya mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na kujiridhisha kuwa itakuwa ni hasara kuendelea na ujenzi wa mradi huo. Hivyo imeamriwa mradi huo uuzwe kwa wawekezaji wengine.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa mfuko unaendelea na hatua na taratibu za wawekezaji wenye nia ya kutwaa eneo hili kwa nia ya kununua mradi huo waweze kupewa.