Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 67 2025-04-14

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhamasisha watumiaji wa Tanzania kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya bidhaa hizo kupitia mikakati mbalimbali ya ukuzaji biashara ndani na nje ya nchi. Mikakati hiyo ni pamoja na:-

(i) Kuanzishwa kwa rajamu/chapa maalum ya bidhaa ya Made in Tanzania ambayo itatumika kwa lengo la kutambulisha na kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini katika masoko yetu ya ndani na pia yale ya Kimataifa;

(ii) Kuratibu maonesho ya bidhaa za Tanzania (TIMEXPO) na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika kila mwaka, ikiambatana na utekelezaji wa kampeni ya “Nunua bidhaa za Tanzania, Jenga uchumi wa Tanzania” ambapo wazalishaji, wasambazaji, wanunuzi pamoja na watoa huduma za usaidizi kutoka sekta za umma na binafsi hushiriki.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini kupitia majukwaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na niliyoyataja hapo juu. Aidha, niwaombe Waheshimiwa Wabunge kuwa mabalozi kwa kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji wa ndani na kuhamasisha jamii ya Watanzania kuendelea kutumia bidhaa hizo. Ninakushukuru.