Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 66 2025-04-14

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inatekeleza Mradi wa Ununuzi wa Magari na Vifaa vya Kuzimia Moto na Uokoaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100 kutoka kampuni ya NAFFCO FZCO iliyopo Dubai. Mradi huo utawezesha kupatikana kwa vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari 150 ya kuzima moto na uokoaji yatakayosambazwa nchi nzima ikiwemo Wilaya ya Nyang’hwale.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali itaendelea kuliimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kulipatia vitendea kazi ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Ahsante.