Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 5 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 65 | 2025-04-14 |
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:-
Je, lini TANAPA watatumia vizuri fursa za Misitu waliyonayo kunufaika na Biashara ya Carbon kama nchi nyingine zinavyonufaika?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ikiwa ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zenye maeneo ya misitu inatambua uwepo wa biashara hii na tayari imeanza kuchukua hatua ili kuhakikisha upatikanaji wa manufaa yanayotokana na biashara ya hewa ukaa. Katika kutekeleza azma hiyo, Menejimenti ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania iliwasiliana na Kituo cha Uratibu wa Biashara ya Hewa Ukaa cha Taifa kilichopo katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine ili kupatiwa Mwongozo wa Biashara ya Hewa Ukaa ulioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, kufuatia mwongozo huo, Shirika limebainisha hifadhi zenye fursa ya biashara hii katika maeneo ya kaboni ya kwenye udongo, Kaboni ya kwenye miti na Kaboni ya kwenye maji. Kwa sasa taratibu za kuandaa mikataba ya makubaliano baina ya TANAPA na makampuni yanayohusika na biashara ya hewa ukaa zinaendelea na baada ya mikataba hiyo kukamilika, TANAPA itaweza kunufaika na biashara ya hewa ukaa kama nchi nyingine zinavyonufaika na biashara hiyo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved