Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 64 2025-04-14

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itatafsiri upya Liquor and Intoxication Act, 1968 ili kutoa fursa kwa Wakulima wa Korosho kupata kipato kwenye Gongo ya Mabibo?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Intoxicating Liquors Act, inaweka utaratibu wa kuwasimamia watengenezaji na wauzaji wa pombe za asili. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, mtu yeyote anayekusudia kutengeneza au kuuza pombe ya asili anapaswa kuomba leseni kwa Mamlaka husika ya Serikali za Mitaa. Aidha, kwa mujibu wa Sheria hii Gongo sio miongoni mwa pombe za asili (local liquor) kama ilivyotafsiriwa katika kifungu cha 3 cha Sheria husika.

Mheshimiwa Spika, Pombe aina ya Gongo, Machozi ya Simba, Moshi au Umeme kama ilivyotafsiriwa na kifungu cha 2 cha Sheria ya Kudhibiti Utengenezaji wa Pombe za Asili, Sura 384 (Traditional Liquor (Control of Distillation) Act) inaweza kutengenezwa ikiwa mtengenezaji ana leseni iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria ya Kudhibiti Pombe za Asili Sura ya 384. Leseni hiyo hutolewa na Waziri mwenye dhamana ya viwanda. Aidha, ni kosa la jinai kuzalisha pombe ya asili ikiwemo Gongo bila leseni. Hivyo wakulima wa korosho wanayo nafasi ya kujiongezea kipato kupitia gongo ya mabibo ikiwa wataomba leseni ya kuzalisha pombe hiyo kutoka Wizara husika.