Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 63 2025-04-14

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:-

Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwasaidia matibabu ya ngozi watu wenye Ualbino kutokana na Ugonjwa wa Saratani ya Ngozi kuongezeka?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto wanazokabiliana nazo watu wenye ualbino. Serikali imechukua hatua kadhaa kusaidia matibabu na kinga ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino kwa kutekeleza yafuatayo:-

(i) Kuanzisha vituo maalum vya uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi katika hospitali mbalimbali nchini ili kuhakikisha watu wenye ualbino wanapata huduma hizi kwa urahisi;

(ii) Kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa vifaa kinga ikiwemo mafuta maalum ya kujikinga na jua ambayo yamejumuishwa kwenye bidhaa za afya zinazoagizwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD);

(iii) Serikali imeandaa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu Wenye Ualbino, unaolenga kuboresha hali ya maisha ya watu wenye ualbino kwa kuimarisha huduma za afya, elimu na ulinzi dhidi ya saratani ya ngozi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.