Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 62 2025-04-14

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya utafiti wa kina nchi nzima wa kusaidia kutambua kuwa ni saratani zipi zinaongoza katika Kanda ya Ziwa na kubaini kuwa saratani ya kibofu cha mkojo, saratani ya mji wa uzazi wa akinamama, saratani ya damu, macho na figo ndiyo zinazoongoza.

Mheshimiwa Spika, aidha, wataalam wamekusanya sampuli za damu 9600 za watu ambao hawana saratani ili kulinganisha na sampuli za damu za wenye saratani. Utafiti huu utasaidia kubaini chanzo cha hizo saratani. Hivyo kwa sasa bado utafiti unaendelea na visababishi vinavyosemwa bado ni nadharia tu kutokana na shughuli za kijamii katika maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa mpango wa kudhibiti ongezeko umejikita katika kutoa elimu ya afya kwa viashiria vinavyodhaniwa pamoja na kuzingatia mkakati wa kitaifa wenye maeneo saba yaliyoainishwa ili kudhibiti viashiria vya saratani.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)