Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Water and Irrigation Wizara ya Maji 61 2025-04-14

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji Vwawa – Mlowo pamoja na Mradi wa Ukarabati wa Vyanzo vya maji Mwansyana na Mlowo. Utekelezaji wa Mradi huo wa Vwawa – Mlowo umefikia wastani wa 79% wakati Mradi wa Ukarabati wa Mwansyana – Mlowo umefikia wastani wa 94%. Tayari baadhi ya maeneo ya Mlowo Forest, Izyla, Saganoti, Malenje, Segerea, Mbimba, Ilolo Shule na Namleya yameanza kupata huduma ya maji kupitia miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2025 na kunufaisha wananchi wapatao 36,744 waishio kwenye Maeneo ya Hasamba, Ilolo, Vwawa, Ichenjezya, Mlowo Mabatini, Mlowo Mjini, Tazara, Kiwandani, Ichenjezya, Isangu, Hasanga, Mlowo Forest, Izyla, Saganoti, Malenje, Segerea, Mbimba, Ilolo Shule na Namleya.