Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Water and Irrigation Wizara ya Maji 60 2025-04-14

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:-

Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Mradi wa Kutoa Maji Ziwa Victoria kwenda Mikoa ya Singida na Dodoma unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025. Mradi huo utakapotekelezwa unatarajia kuhudumia Miji ya Singida na Dodoma pamoja na vijiji vilivyo ndani ya umbali wa kilometa 12 kutoka kila upande wa bomba kuu ikiwemo Vijiji vya Wilaya ya Mkalama. Aidha, vijiji vitakavyokuwa nje ya kilometa 12, Serikali itavipelekea huduma ya Mradi wa Ziwa Victoria baada ya awamu ya kwanza ya mradi huo kukamilika na kuanza kutoa huduma.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa jumla ya vijiji 29 kati ya 70 vya Wilaya ya Mkalama vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia mtandao wa bomba wakati vijiji 41 vinapata huduma ya maji kupitia point source na pampu za mkono. Vilevile, Serikali inaendelea na utekelezaji wa jumla ya Miradi Sita ya Mbigigi, Isene – Matongo, Mdilika, Tumuli, Singa na Mwangeza ambapo kukamilika kwake kutanufaisha wananchi zaidi ya 15,000 waishio kwenye Vijiji Saba vya Wilaya ya Mkalama.