Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 59 2025-04-14

Name

Khamis Yussuf Mussa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Primary Question

MHE. KHAMIS YUSSUF MUSSA aliuliza:-

Je, lini Serikali itainufaisha Zanzibar katika matumizi ya nishati ya gesi kutumika katika magari?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mwezi Februari, 2022, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) iliingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ambapo kupitia ushirikiano huo masuala mbalimbali yamekuwa yakifanyika ikiwemo kubadilishana ujuzi na utaalam. Katika ushirikiano huu, suala la kupeleka gesi asilia Zanzibar ni mojawapo ya agenda kuu. Pande zote mbili bado zinaangalia namna bora ya kufikisha gesi asilia Zanzibar ili iweze kupatikana kwa bei rafiki kwa watumiaji.