Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Finance and Planning Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 58 2025-04-14

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER L. MIDIMU K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani kujenga miundombinu ya maji shuleni ili kuepuka milipuko ya magonjwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, shule 5,311 za Sekondari zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 2,960, visima shule 1,217 na wanaovuna maji ya mvua ni shule 1,134. Aidha, shule 20,509 za msingi zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 10,965, visima shule 4,966 na shule zinazovuna maji ya mvua ni 4,578.

Mheshimiwa Spika, Mikakati ya Serikali ya kujenga miundombinu ya maji shuleni ili kuepuka milipuko ya magonjwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa: -

(a) Ujenzi wa shule mpya unajumuisha miundombinu ya maji inayohusisha kuvuna maji ya mvua, kuunganisha na mifumo ya Mamlaka za Maji na kuchimba visima;

(b) Ujenzi wa miundombinu ya vyoo unajumuisha wa miundombinu ya maji tiririka; na

(c) Kutumia sehemu ya fedha ya ruzuku ya uendeshaji wa shule kukarabati miundombinu ya maji.