Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 57 2025-04-14

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatatua changamoto ya uhaba wa Walimu katika Halmashauri ya Mji Nanyamba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa spika, Serikali inatambua changamoto ya uhaba ya walimu katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali imeajiri walimu 15,925 ambapo walimu 27 na mafundi sanifu maabara wawili wamepangwa Halmashauri ya Mji Nanyamba. Serikali itaendelea kuajiri walimu na kuwapanga katika shule zenye upungufu katika Halmashauri ya Nanyamba. Ahsante.