Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 56 2025-04-14

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:-

Je, lini Serikali italitengeneza na kulitangaza Daraja la Mungu la kihistoria lililopo Wilaya ya Rungwe ambalo lipo katika hali ya kutotunzwa?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Daraja la Mungu lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe limetokana na mabadiliko asili ya miamba na kulifanya kuwa ni daraja ambalo halikuwahi kutengenezwa na mwanadamu hivyo kuwa kivutio cha utalii wa ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na sababu hiyo, daraja hili haliwezi kutengenezwa kwa njia za kibinadamu hivyo litaendelea kuwa la asili kama lilivyo kwani halitumiki kwa shughuli nyingine za kibinadamu isipokuwa kwa utalii pekee.