Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 5 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 55 | 2025-04-14 |
Name
Aziza Sleyum Ally
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati na shule yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi Nzega?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua mchango wa nguvu za wananchi hususan katika uanzishaji wa miradi ya kijamii kama shule na vituo vya kutolea huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2023/2024, Serikali ilipeleka shilingi bilioni 64 kwa ajili ya maboma ya zahanati na shule. Katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi milioni 835 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma sita ya zahanati na madarasa 17 yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi katika Halmashauri ya Nzega.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maboma ya zahanati na madarasa yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi ili kusogeza huduma za afya ya msingi na elimu karibu na wananchi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved