Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Question to Prime Minister

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Home Affairs Maswali kwa Waziri Mkuu 1 2026-05-14

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Gender

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali kwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, Askari ni kundi kubwa muhimu sana katika jamii yetu na kwa mazingira ya kazi yao kuumia kazini ni rahisi sana. Ni kwa nini, sasa Serikali isione haja, na pengine wakati umefika sasa kwa Askari hao kujiunga na Mfuko wa Fidia Kazini (Workers Compensation Fund – WCF) ili Askari hawa wanapopata majanga au kuumia kazini mfuko uweze kuwatibia ili na wao wanufaike na mafao yanayotolewa na mfuko huo? Ahsante.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Gender

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ninakushuru kwa nafasi hii ya kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama ambavyo Mheshimiwa Mchafu amesema kwa aina ya majukumu wanayofanya vijana wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuumia kazini ni jambo linalotarajiwa. Kwa sasa, utaratibu unaotumika kuhusu masuala ya fidia kwa vyombo vya ulinzi na usalama uko kisheria na unazingatia sheria na kanuni ambazo zinawataka kwamba masuala ya fidia yafanywe kwa taratibu za kiulinzi na usalama.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tunapokea wazo la Mheshimiwa Mbunge, Serikali itafanya tathmini kuona kama tunaweza tukapanua wigo kutoka kwenye mifuko ya WCF na kuweza ku-accommodate watumishi walioko kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Jambo hilo litakapokuwa limekamilika, tutaweza kulitaarifu Bunge lako Tukufu kupitia taratibu zetu za Kibunge, kama jambo hilo litaweza kutekelezeka kwa utaratibu huo au kuboresha utaratibu unaotumika sasa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Additional Question(s) to Prime Minister