Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Question to Prime Minister

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Maswali kwa Waziri Mkuu 1 2026-04-02

Name

Rose Cyprian Tweve

Gender

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, nipo. Nipo Mheshimiwa.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali ili kuhakikisha inapambana na kutokomeza Malaria nchini, ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 6.5. ikaenda pale Kibaha kuhakikisha wananunua viuadudu na ikazitaka halmashauri zote 184 nchini kufika pale Kibaha kuchukua zile dawa na kupeleka kwenye maeneo yao na kuhakikisha wananyunyiza mazalia ya mbu.

Mheshimiwa Spika, jambo la kusikitisha, tumefika kiwandani pale, kuna baadhi ya halmashauri hazijatekeleza agizo hilo, na imelazimu kile kiwanda kuchukua zile dawa ambazo Serikali ilinunua na kuzifungia stoo.

Mheshimiwa Spika, sasa swali langu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, nilitaka kujua tamko la Serikali kwa halmashauri hizi ambazo zimefanya uzembe wa kutotii agizo hili la Serikali na kusababisha adha kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, pia utakubaliana na mimi kuwa tatizo la Malaria bado linaendelea kupoteza maisha ya Watanzania kwa kusababisha vifo hususan kwa wanawake na watoto. Ninakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Gender

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwepo na agizo na uelekeo huo wa Serikali katika jitihada za kupambana na Malaria kuhakikisha kwamba kunakuwepo na dawa hizo ambazo Serikali imefanya jitihada za kuzinunua, na dawa hizo zipo. Lengo ilikuwa ni kupelekwa kwenye halmashauri zote ili ziweze kuchukua hatua ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji huo na kwa umakini wake hasa hasa wa kuzingatia suala la kutokomeza Malaria, jambo ambalo linawaathiri sana hasa wakina mama pamoja na watoto wadogo.

Mheshimiwa Spika, ninakumbuka jambo hili likiwa limejadiliwa ndani ya Serikali, na taarifa zilizokuwepo ilikuwa yafanyike mafunzo katika ngazi za halmashauri kuhusu utekelezaji wa jambo hilo. Pia, kulikuwepo angalizo la ratiba kwamba jambo hilo liwe linatekelezwa mwezi Juni na kuendelea pale ambapo maeneo mengi ndani ya nchi yetu yanakuwa hayana mvua.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia swali la Mheshimiwa Mbunge na maelezo hayo aliyoyatoa, basi nitoe maelekezo kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kufuatilia halmashauri zote ambazo bado hazijatekeleza wajibu huo ili waweze kuzingatia kalenda hiyo iliyotolewa ya kufanya zoezi hilo ifikapo Juni, 2026.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, halmashauri zote ambazo walikuwa bado hawajatekeleza wajibu huo, wafanye hivyo kati ya sasa na ifikapo Mei, 2026, wote wawe wameshakusanya dawa hizo ili ifikapo Juni, 2026 na kuendelea, waweze kutekeleza wajibu huo wa kuzisambaza dawa hizo katika hatua hiyo ya kutekeleza zoezi la kutokomeza Malaria. (Makofi)

Additional Question(s) to Prime Minister