Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Eng. Mwanaisha Ng’anzi Ulenge (1 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana Mheshimiwa kwa nafasi ya kuchangia. Niendelee kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuendelea kutoa mchango katika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote niendelee kumpongeza sana Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa aliyokuwa nayo ya kusongesha maendeleo ya Taifa letu. Hakika kupitia sekta hii ya mawasiliano na teknolojia ya habari, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha vision kubwa, maono makubwa ya namna ambavyo anatamani kuibadilisha Tanzania na kuweza kunufaika ipasavyo na sekta hii ya mawasiliano na teknolojia ya habari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika natoa pongezi nyingi sana kwake na kwa nini ninazungumza hivi kwamba ana maono makubwa Dkt. Samia Suluhu Hassan?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia namna ambavyo anasisitiza kuhusu uchumi wa kidigitali na taarifa ambazo Afrika inakwenda kunufaika na uchumi wa kidigitali, utamwangalia Dkt. Samia Suluhu Hassan kumuona ni Rais wa aina gani. Africa Digital Economy inatarajiwa mwaka 2025 kufikia thamani ya bilioni 180 na inatarajiwa itakapofikia 2050 uchumi wa kidigitali wa Afrika utafikia bilioni 712. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiuhalisia kwa uelewa wangu mdogo Wizara hii ni Wizara wezeshi. Ni Wizara wezeshi ambayo inawezesha kurahisisha shughuli na utendaji wa Serikali, lakini kuwezesha kuwa kama kichocheo cha kuchochea uchumi kupitia sekta mbalimbali za kiserikali na sekta binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze sana Wizara hii inayoongozwa na mtu bingwa kabisa shemeji yangu mwenyewe Jerry Silaa. Hakika kwa programu au kwa Mradi wa Digital Economy, Tanzania na uchumi wa kidigiti mradi huu ambao ni wa milioni 150 hakika ni mradi ambao unakwenda kufanya mapinduzi makubwa katika Taifa letu. Niwapongeze sana sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wako Engineer Maryprisca pamoja na watendaji wote wa Wizara wakiongozwa na Katibu Mkuu kwa kuhakikisha mradi huu wa Tanzania ya Kidigiti unakwenda kusimama sawasawa na umeweka msingi mzuri wa kurahisisha shughuli za Serikali pamoja na kukuza biashara ya uchumi wa kidigitali nchini Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa uchumi wa kidigiti pamoja na uwepo wa Tume ya TEHAMA umeweka msingi mzuri wa kutumia kundi kubwa la vijana ambalo ndiyo population kubwa nchini kuhakikisha inakwenda kuzalisha ajira mbalimbali kwa vijana wa Kitanzania. Ukiliangalia soko la Africa e-Commerce pamoja na uchumi wa kidigitali unatarajiwa kuzalisha fursa za ajira milioni 200. Kwa hiyo, kuna wimbi kubwa la fursa katika sekta hii ya habari na teknolojia. (Makofi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika mradi wa uchumi wa kidigiti umefanya mambo makubwa katika Tanzania yetu na umeweka msingi mzuri ambao matarajio yangu kwa sababu mradi huu unakwenda kukamilika, ninaomba sana kuhakikisha uendelevu wa mradi huu. Mradi huu ambao umekwenda kuweka base nzuri ya kuhakikisha tunakwenda kukuza muunganiko wa kimtandao (internet connectivity) nchini ambalo ni jambo la muhimu katika kurahisisha e-Commerce nchini Tanzania, hakika tunahitaji mwendelezo wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeona mradi wa Tanzania ya kidigiti ambao umeweza kutengeneza ile sehemu maalumu ya data center ya kuhifadhi data zetu katika sehemu moja ambayo ni salama na kuweza kulinda data zetu zisiweze kuhamishwa kirahisi kwenda mataifa mengine. Hii nayo ni biashara ndani yetu, data zetu zimekuwa zikichukuliwa kirahisi mtu yoyote kutoka mataifa mengine amekuwa akiingia na kuchukua data kirahisi. Maana yake Tanzania tulikuwa tuko uchi, yoyote anaweza kutafuta chochote Tanzania na akaweza kupata lakini kwa miundombinu ambayo imewekwa katika data center, ambayo imegharimu bilioni 60 hakika ni mapinduzi makubwa ya Tanzania na Uchumi wa kidigitali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana, niombe sana, sekta hii ya kuhifadhi data zetu na zisiibiwe ni sekta muhimu kwa ulinzi wa Taifa letu. Naomba sana muendelee kuwekeza nguvu katika jambo hili la uhifadhi wa data zetu na vilevile kuongeza nguvu katika sekta hii ya kuhakikisha inaunganika kama mlivyopanua wigo wa kuanzisha dirisha la shughuli za kiserikali kwa kupitia mradi huu wa Tanzania ya Kidigiti, mpanue wigo kama ambavyo mmefanya na NECTA tayari, kama ambavyo mmefanya na sekta ya madini tayari, kama ambavyo mmeunganika na NIDA kwa maana ya kwenda kuanzisha zile Jamii Namba, Jamii Exchange, N-card na soft card tunatamani muendelee kuingia kwenye sekta ya ulinzi pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuona pale Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Bashungwa anaona. Mkaunganike tuone namna ambavyo tunapokuwa tunamiliki silaha mfumo unakwenda kutambua wananchi wote wanaomiliki silaha, wananchi wote ambao wanafariki silaha zile zinahamishika vipi? Silaha zile zinarithishwa vipi. Ni kwa kupitia mfumo huu wa kidigitali tunaweza kuendeleza ku-enhance security ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie suala zima la hisa ambazo zimewekwa na wananchi wa Tanzania kwa kupitia Kampuni ya Vodacom. Nimependa maono ya wenzangu ambao wametangulia kuyatoa na ninaomba nisisitize kwamba dhamira na lengo la Mtanzania mmoja kuweka fedha zake pale ni kupata faida. Sasa wakati yote yanakwenda kufanyika mimi binafsi sitaelewa zaidi ya kuona ni namna gani ninapata fedha zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mantiki hiyo ninaomba Waziri atakapokuja ku-wind up aje na kusema ni namna gani Watanzania watapata fedha zao mengine yote ni longolongo. Tunaona ni namna gani watu wame-invest, end of the day miaka 10-15 nataka kupata riba yangu ambayo kama ninavyapata UTT, ambayo kama ninapata kwenye treasury bond na huku nione the return of the investment ambayo mimi nimeiwekeza ndania ya miaka 10 niione kiganjani kwangu. (Makofi)

Kwa hiyo, yote yafanyike lakini at the end of the day tuone wananchi wamepata fedha zao mikononi na hiyo ndiyo itakuwa solution, whether itaendelea ama sheria itabadilishwa end the day we need money kwenye mikono yetu na Watanzania tuliwekeza kwa namna njema ya kuweza kurudisha fedha hizo kwenye mikono yetu. Mheshimiwa Waziri hili ninaamini unaliweza, uwezo wako hauna mashaka, tunakutegemea na tunakutarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja kwa 100% ahsante sana. (Makofi)