Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Arif Suleiman Premji (1 total)

MHE. ARIF S. PREMJI aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara kutoka Kijiji cha Hiyari kwenda Mkunwa - Makao Makuu ya Halmashauri kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Arifa Suleiman Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Hiyari – Mkunwa kilometa 10 ni sehemu ya Barabara ya Mkoa ya kutoka Msijute – Mnima – Nanyamba yenye urefu wa kilometa 78.75, inayohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inajengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ambapo hadi sasa jumla ya kilometa mbili zimejengwa kwa kiwango cha lami kuanzia eneo la Msijute. Sehemu iliyobaki ya barabara hii itajengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.