Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Rose Vicent Busiga (5 total)

MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya, Kata ya Nhomolwa – Mbogwe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Nhomolwa kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Kituo hiki kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga jengo la kutolea huduma za nje (OPD) na majengo mawili ya wodi ya kulaza wagonjwa.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe ilipeleka shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya mtumishi ya two in one, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma mwezi Oktoba, 2023.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la maabara. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Nhomolwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya, Kata ya Nhomolwa – Mbogwe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Nhomolwa kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Kituo hiki kilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga jengo la kutolea huduma za nje (OPD) na majengo mawili ya wodi ya kulaza wagonjwa.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe ilipeleka shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje na nyumba ya mtumishi ya two in one, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma mwezi Oktoba, 2023.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mbogwe imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la maabara. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Nhomolwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Bukombe hadi Katoro kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Bukombe – Katoro yenye urefu wa kilometa 58.20 kwa kiwango cha lami, unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Awamu ya kwanza inahusisha sehemu ya Bukombe (Ushirombo) hadi Bwenda (kilometa 5.3). Zabuni za kumpata mkandarasi zimefunguliwa tarehe 20 Januari, 2025 na kazi ya tathmini ya zabuni hizo inaendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa sehemu ya pili ya kutoka Kashelo hadi Nyikonga (kilometa 10.4) pamoja na Daraja la Nyikonga iko katika hatua ya majadiliano. Mkataba wa kazi unatarajiwa kuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Februari, 2025. Kwa sehemu zilizobaki za Bwenda – Kashelo (kilometa 16.3) na Nyikonga – Katoro (kilometa 26.2), Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi.
MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itawalipa mafao yao mashujaa wa Vita vya Kagera na Uganda?
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mashujaa wote waliopigana vita vya Kagera na waliostahili malipo ya viinua Mgongo na Pensheni walikwishalipwa na wengine wanaendelea kulipwa kwa mujibu wa Sheria ya Pensheni na Viinua Mgongo ya Mwaka 1966; ikiwemo pia malipo ya ulemavu na ustaafu.

Mheshimiwa Spika, kundi ambalo lilishiriki vita na halikuwa limeajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya vita lilipewa nafasi ya kujiunga katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufuata taratibu. Kwa wale walioamua kutojiunga na wale waliokosa sifa katika kundi hilo walilipwa kifuta jasho, Ahsante Nyerere kiasi cha Shilingi 5,000 ambayo kwa wakati huo ilikuwa pesa ya kutosha na kurejeshwa makwao.

Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali kuhusiana na maveterani wa Vita ya Kagera. Miongoni mwa changamoto hizo ni madai ya mavetenari wote kuingizwa katika daftari la Pensheni licha ya kuwa baadhi yao hawakidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria, madai kuwa pensheni ni ndogo na maombi ya kupewa Bima ya Afya.

Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto hizo, Wizara imeandaa mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Pensheni na Viinua Mgongo ya mwaka 1966 na kuiwasilisha Serikalini, yakijumuisha maveterani waliopigana Vita vya Kagera. Aidha, Wizara imewasilisha Serikalini mapendekezo ya kuona uwezekano wa kuwaingiza maveterani waliopigana Vita vya Kagera kwenye utaratibu wa bima ya afya.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. ROSE V. BUSIGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Runzewe Mashariki – Bukombe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Bukombe imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Msonga kilichopo Kata ya Runzewe Mashariki. Mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 413.08 zimepelekwa na kutekeleza ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara na jengo la kliniki ya mama, baba na mtoto (RCH). Majengo yote yamekamilika na yanatumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imetoa shilingi milioni 164.05 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi (maternity) na jengo la upasuaji. Ujenzi wa majengo haya umefikia 85%. Aidha, katika mwaka 2025/2026 Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri imetenga shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kufulia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa wa miundombinu ya msingi ikiwemo wodi ya mama na mtoto katika Kituo cha Afya Msonga katika Kata ya Runzewe Mashariki Ahsante.