MHE. KAKULU B. KAKULU aliuliza: -
Je, lini upanuzi wa Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala Rangi Tatu – Kongowe unatarajiwa kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) iliingia mkataba na Mkandarasi M/S STECOL Corporation kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala Rangi Tatu – Kongowe yenye urefu wa kilometa 3.8. Mkataba ulisainiwa tarehe 19 Agosti, 2025 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 15. Kazi za ujenzi zinatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu 2026.