Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Sara Msafiri Ally (1 total)

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Sara Msafiri Ally, Mbunge wa Mvomero, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo – Kisaki inajumuisha barabara ya Mkoa ambayo inaanzia Sangasanga – Langali – Luale – Kikeo yenye urefu wa kilometa 59.16 inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuhakikisha barabara hiyo inapitika majira yote ya mwaka na kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi, Serikali imeendelea kufanya matengenezo mbalimbali hususan sehemu korofi kwa kuijenga kwa kiwango cha lami na zege ambapo jumla ya kilometa 13.19 zimejengwa na kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali pamoja na hatua hizo, inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo ili kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.