Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Kellen Rose Rwakatare (1 total)

MHE. KELLEN R. RWAKATARE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kutoka Daraja la Lumemo - Mbingu – Chita?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya kuanzia Daraja la Lumemo – Mbingu – Chita ni sehemu ya barabara ya Ifakara – Njombe Border yenye urefu wa kilometa 220. Ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa, ujenzi umeanza sehemu ya Ifakara – Mbingu, kilometa 62.5. Aidha, kwa sehemu ya Mbingu – Chita, urefu wa kilometa 37.5, mkandarasi amepatikana na taratibu za malipo ya awali advance payment zinaendelea ili aweze kuanza kazi, ahsante.