Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Mecktridis Fratern Mdaku (1 total)

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA K.n.y. MHE. MECKTRIDIS F. MDAKU aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Ifakara – Lupilo hadi Malinyi kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mecktridis Fratern Mdaku, Mbunge wa Malinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Ifakara – Lupilo hadi Malinyi kwa kiwango cha lami kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu ilikuwa ni kukamilisha ujenzi wa daraja la Magufuli (meta 384) katika Mto Kilombero pamoja na barabara ya maingilio (kilometa 9.143) ambalo lilikuwa kikwazo kikubwa katika barabara hii.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa, Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Ifakara – Lupilo – Mtimbira yenye urefu wa kilometa 112 ambapo taratibu za malipo ya awali kwa Mkandarasi ili aweze kuanza kazi zinaendelea. Kwa sehemu zilizobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.