MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ninakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Guta, kwenye Jimbo la Bunda Mjini, kuna eneo la Tairo ambalo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji na wananchi wameshalipwa fidia. Eneo hili limekaa wazi zaidi ya miaka 14. Naibu Waziri ameenda kulitembelea eneo lile, eneo ambalo ni very potential, liko karibia na Ziwa na lipo kwenye lami. Je, ni lini sasa wataletwa wawekezaji, wajenge viwanda ili akina mama wa Bunda na Vijana wa Bunda waweze kupata ajira? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Bulaya, amekuwa akinisumbua sana kuhusu ile Bunda SEZ, ambayo kimsingi ni mojawapo ya vipaumbele vya Serikali. Kama tunavyotambua, Rais amesisitiza kwamba tunaenda kuanzisha kongani za viwanda, lakini mojawapo ya mkakati wetu sasa hivi tunaenda ku-promote uwekezaji kwenye maeneo ya SEZ. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunda ni mojawapo ya meneo ambayo kimsingi ni mkakati wa Serikali na katika bajeti yetu ya mwaka huu imo, na tunaenda kutenga eneo kwa ajili ya uwekezaji wa vijana. Ninaomba nimhakikishe Mbunge kwamba suala la Bunda SEZ tumelipa kipaumbele. Ahsante.