Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Revocatus Chipando Clayton (3 total)

Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/2027–2050/2051, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/2027–2030/2031 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/2027; na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Katika Muda wa Kati ya 2026/2027 hadi 2028/2029.
MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii adhimu ili niweze kuchangia mawili matatu kwenye Mpango wa Miaka 50 ya Maendeleo ya Nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniweka hai mpaka leo hii kwa sababu kampeni zangu zilikuwa na heka heka nyingi. Pili, namshukuru Mwenyekiti wangu wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupitisha jina la Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo). Watu wengi waliongea lakini sasa hivi nadhani akikaa anaona raha kwa sababu anaona mambo yanayoendelea Jimbo la Kigoma Mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, ninawashukuru sana wananchi wa Kigoma Mjini walipiga kura nyingi na walinipa moyo tangu ninazindua kampeni katika Jimbo la Kigoma Mjini. Umati uliokuwa unanifuata nyuma, ni wafuasi ambao walinionesha wazi kwamba tunakupeleka Bungeni. Ninataka niwaahidi kwa uwezo wangu na elimu yangu niliyonayo, hii ndiyo ajira yangu kubwa ya mwisho Ubunge, nitawatumikia kwa nguvu zangu zote kuhakikisha ninakuwa Mbunge bora katika Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukurani, ninaomba nimpongeze Waziri wangu mzee wangu Mheshimiwa Profesa Kitila. Mheshimiwa Profesa Kitila ni moja kati ya ma-genius. Nilikuwa na Mheshimiwa Profesa Kitila, zamani tulikuwa naye CHADEMA, tulifukuzwa wote kama anakumbuka, tulifanya press pale pamoja, kikundi chetu, sasa tuko kwenye chama kikubwa, Chama Cha Mapinduzi. Mungu akujalie sana uendelee kutusaidia kwa mawazo haya ambayo umeyaleta katika mpango huu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka haraka ninaomba nijikite katika upande wa vijana. Nimeona mambo mengi sana yameelezewa namna bora kuweza kuwasaidia vijana katika Mpango huu wa miaka 50 ya Maendeleo ya Nchi yetu ya Tanzania. Vijana hawataki konakona, vijana wanataka hela, ninaomba sana mpango huu upunguze kona kona kwenye namna ya kumfikishia kijana hela, kijana anataka pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitawaambia ukweli, wakiangalia mara nyingi sana tunakuwa tunasisitiza hapa vijana wajiajiri, wazee kujiajiri lazima uwe na hela, unajiajirije, ukitaka kujiajiri, ukiniambia mimi wakati niko nje ya Bunge Baba Levo jiajiri, najiajirije labda nifungue biashara yangu, biashara naifungua na nini? Tupunguze masharti ya vijana kuweza kukopa, tunaweka masharti magumu, mtu kama Linex anataka kukopa unamwambia alete hati ya nyumba, Linex ana nyumba? Lazima tuweke masharti ambayo yataendana na vijana tulionao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu amemaliza chuo, ndiyo kwanza anahaha na documents zake kutafuta ajira unamwambia jiajiri, anajiajiri kwa mfumo gani, unamwambia bwana tafuta mikopo, anaenda kwenye mikopo, benki zetu tunazijua zina vigezo ambavyo hivyo vigezo vinamtaka awe na mali ambayo ameshika aiweke kama dhamana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutafute njia sahihi ya hawa vijana pesa ziwafikie bila njia ngumu wanazopitia. Mimi nitawaambieni ukweli, mimi ni mfano, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akituwekea wasanii pesa kwa ajili ya kukopa, tumeenda kukopa, nimeenda kukopa milioni 100, masharti niliyokutana nayo pale cha kwanza niwe na mali kama gari au nyumba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikajiuliza kuhusu wasanii wa singeli hivi hawa watatoboa kweli kwenye huu mpango. Kwa tafsiri hiyo, hata hizi pesa ambazo nimeona Waziri Mheshimiwa Makonda amepewa shilingi bilioni mbili, wapunguze masharti ya namna vijana kuzifikia hizo pesa. Wakiwawekea masharti magumu, tenda watachukua wale wasanii ambao tayari wameshakuwa matajiri wana hela na wale wenye vipaji wa chini zile pesa hazitawafikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wanataka pesa bila kona kona na ndiyo maana vijana wengi wanabeti kwa sababu ukibeti unamuua Simba mechi ikiisha unachukua hela yako unaendelea na maisha mengine. Kwa hiyo kwenye hili naomba sana Mheshimiwa Waziri aweke mfumo ambao atawasaidia vijana kupata pesa kwa urahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, tunazungumzia Mpango wa Miaka 50 ya Maendeleo ya Nchi yetu ya Tanzania, ni lazima tuwazungumzie wafanyabiashara wadogo wadogo. Nitatoa mifano, nimezurura sana. Siku moja nilinunua nguo Uturuki za watoto wangu, mimi nina watoto watano nikawanunulia kila mtoto nguo tatu tatu, zikawa kama 15 hivi nikapitia Dubai nikashuka Dubai nikaa Dubai siku tatu, sikudaiwa wala sikuzuiliwa pale airport. Nilivyokuja na zile zile nguo nilivyoshuka nazo Airport ya Tanzania, wakaniambia ninatakiwa nizilipie ushuru nguo za watoto wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo lazima tutengeneze, hii ikanipa picha kwamba wafanyabiashara wadogo wadogo kuna namna ambavyo wanafinywa kiasi kwamba hata kile kidogo alichonacho kinaondoka. Mfanyabiashara ana simu mbili, simu tatu mwacheni apite, kama kunaonekana kuna ugumu wa kufuta hizi kodi ndogo ndogo si dhahabu zipo tuuze tu, tupunguze hizi kodi ndogo ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana yazingatiwe haya kwa sababu, kama tunawasaidia wawekezaji wakubwa lazima tuwakumbuke na hawa wawekezaji wadogo wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtu anaweza kwenda na simu tano Dubai akapita bila kuulizwa chochote kwa nini akipita nazo hapa kwetu inakuwa tatizo? Twendeni tukambane sokoni wakati anauza, tupunguze mauzo ya cash tuweke katika mfumo, watu watumie kadi, watumie kulipa kwa digital, mtaiona hela. Nimeenda China mtu anauza bamia anakupa Alipay una-scan hela inaingia moja kwa moja kwa Serikali, lakini kiuhalisia kwa mfumo huu wa kuwabana hawa wadogo wadogo watawabana watakufa watatengeneza wakubwa, wakubwa watawanyonya wadogo. Ninaomba sana hilo nalo lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango huu wa mzee Mheshimiwa Profesa Kitila, nimeuangalia nimeona kabisa sasa ni muda muafaka wa kuitangaza Bandari ya Kigoma kuwa ndiyo kitovu cha biashara kwa Kanda ya Ziwa. Kwa sababu sisi ndiyo tuko karibu na Kongo na Kongo ndiyo nchi pekee yenye watu wengi katika ukanda wetu huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kongo bahati nzuri tumepata bahati sijui wana matumbo mazuri wanakula kila kitu ambacho tunakitoa Tanzania tunakipeleka kule. Kwa hiyo, ipo namna ambayo tukiitumia Kigoma, ambayo iko connected na Burundi, Kongo na Zambia kuna nafasi kubwa ya nchi yetu kutengeneza pesa nyingi ambazo zitakuja kusaidia kwenye miradi mingine tofauti tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna bandari yetu pia ambayo sasa hivi inaboreshwa pale. Tunaomba sana mzee wangu Mheshimiwa Profesa Kitila waweke mitambo ya kisasa. Sasa hivi pale gari moja kushushwa mzigo yaani unaona wanahaha wale jamaa utafikiri sijui wanafanya kazi gani. Yaani wanatumia focal lift lakini wanakuwa kama makuli, tunaomba mitambo ya kisasa iwekwe ili kufupisha muda wa kupakia na kupakua mizigo katika Bandari ya Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine yatengenezwe maghala ambayo yatakuwa na baridi ya kuweza kuhifadhi mizigo, nataka niwaambieni ukweli, kuna baadhi ya mazao ambayo yanapatikana Kigoma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi yetu ya Tanzania huwezi kuupata mgebuka wewe, nenda kokote hupati mgebuka, lazima uje pale. Pia tuna chikichi, chikichi ndiyo zao pekee ambalo unaweza kulibadilisha kuwa chochote na nitawaambieni hapa. Chikichi unaweza ukaibadilisha ikawa mawese, ukaibadilisha ikawa mafuta ambayo tunakula tunasema Korie, ukabadilisha lile ganda lake likawa meza, ukibadilisha ule muse wa ndani unaweza ukaubadilisha ukawa sabuni, hili ni zao moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mkuu aliyepita mzee wangu Mheshimiwa Majaliwa alikuja Kigoma katika kupambania hili zao, akasema kila mwananchi wa Kigoma Mjini apande mchikichi kwenye nyumba yake nje. Hilo jambo halijatekelezeka kwa sababu hakuna kiwanda ambacho hawa watu wakishapanda hayo mazao kwenye nyumba zao watapeleka wapi? Tutengeneze kiwanda ambacho kitasaidia zao la chikichi liweze kuokoa uchumi wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasihi sana wamekuwa ni maneno mengi kuhusiana na chikichi. Tunajua Malaysia na Indonesia wamekuwa wakipambana kuhusiana na chikichi na sasa hivi tunaona maendeleo waliyonayo. Nawasihi sana ndugu zangu wataalam, wamesoma sana tulibadilishe chikichi iwe kama watu wa Geita wanavyotumia dhahabu kwa ajili ya maendeleo ya maji wetu wa Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yote tutayasema kama Kigoma hakuna miundombinu mizuri, ni aibu. Ninajua Mheshimiwa Waziri Mkuu anaenda kesho Kigoma kwenye miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi, wakati anatua na ndege apige jicho chini wakati ndege imeshuka kidogo aone vumbi iliyotapakaa katika Mji wa Kigoma Mjini. Ni aibu kuita Kigoma Mjini wakati 85% ni barabara za vumbi, ni aibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini wanatufanyia hivi, kwa sababu kiuhalisia kabisa sisi wakitutumia kama kitovu, hii nchi itapunguza tozo nyingi sana za ajabu ajabu mtaani. Kwa sababu tutaleta pesa, hizo pesa zitasababisha wapunguze tozo nyingi. TRA tozo walizonazo mfanyabiashara akilipa tozo zote anafilisika, hata Bakhresa, kama atalipa zote, zote kwa pamoja, atafilisika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni lazima tuwe na vyanzo ambavyo vitasaidia kuwapunguzia mzigo wafanyabiashara. Nisaidieni Kigoma tuwasaidie kupunguza gap lililopo katika bajeti zetu katika Nchi yetu ya Tanzania, watutengenezee barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri ambao amewaleta sasa hivi ni Mawaziri shupavu, wana speed ya kutosha. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Chipando muda wako umekwisha, malizia.

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ndiyo Mbunge pekee ambaye sitegemei kuteuliwa kuwa Waziri kwa sababu ya elimu niliyonayo. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninawategemea sana, sina wivu na wao lakini mimi ndiyo kiherehere ambaye nitawachomekea na nitawachongea pale ambapo watafanya vitu vya hovyo kwenye Jimbo la Kigoma Mjini, sitowaacha. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawaomba sana Mawaziri watusaidie Jimbo la Kigoma Mjini tupate barabara, tupunguze vumbi. Mheshimiwa Profesa Shemdoe, mzee wangu ameniahidi na nitakesha kwenye ofisi ya mzee wangu, ninaomba anisaidie barabara bila barabara sitarudi humu ndani na kama hataki nirudi asinipe barabara mzee wangu. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027
MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika Hotuba ya Waziri Mkuu na bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Moja, kwa kutupa nafasi vijana. Nimeona Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza lawama kuhusiana na vijana katika Bunge hili. Asilimia kubwa ni vijana. Ametupa nafasi twende tukawasaidie wananchi. Lawama yoyote ambapo tulikuwa tunalaumu kwamba vijana hatupewi nafasi, haya Bunge hili hapa, tuko wengi kuliko watu wenye umri mkubwa. Sasa huu ni muda wa sisi kuweza kuonyesha Tanzania kwamba vijana tunaweza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia idadi kubwa ya Mawaziri wamepewa vijana. Mama amemaliza kwenye hilo. Ni muda wetu wa kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, nimeangalia 97% ya Wabunge wote ambao wameongea katika Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wameongelea barabara. Tafsiri yake ni kwamba suala la barabara ni tatizo, ni kama janga lingine. Ni kwa nini tusifanye maamuzi Bunge hili tukaliweka suala la barabara kama janga la Taifa na tukatafuta namna bora ya kuweza kutatua shida ya barabara? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukimpelekea mkulima mbolea shambani halafu usipompa barabara ya kufikisha hayo mazao ambayo anayatoa shambani kuyaleta mjini, ni sawa na kazi bure. Ukijenga hospitali ya wilaya, usipowapa wagonjwa njia ambayo watapitishwa na hiyo ambulance kwenda hospitali, hiyo ni sawa na kazi bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kigoma Mjini, hospitali ya wilaya ilipojengwa, hakuna barabara ya kuwafikisha watu pale. Ni mashimo, mabonde na kuinama. Tafsiri yake ni nini? Utampeleka mzazi kwenda kujifungua wakati unampeleka unampiga kwenye mashimo, afike kwanza atengenezwe kwanza nyonga uliyovunja kwenye mashimo; haiwezekani. Lazima tufanye maamuzi. Vijana tuko humu ndani, tufanye maamuzi kuhusiana na suala la barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nimwambie ukweli Mheshimiwa Waziri Mkuu. Suala la TARURA kuna mtego huo huwa wanatuingiza; mkenge. Ukisikia wataalam wanakushauri upeleke barabara ya vumbi kwenye jimbo lako, tafsiri yake ni kwamba wamejitengenezea kitengo cha kuwa wanakutana na mkandarasi kila mwaka kuchukua 10%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kwa sababu utatengeneza barabara ya vumbi mwaka huu kwa shilingi milioni 400, ikifika mwezi Desemba mvua zikinyesha, zinazoa milioni 400 yote zinaipeleka ziwani au kwenye mto. Mwaka kesho wanatenga tena milioni 400 kwa ajili ya kujenga barabara ile ile. Wale watu wa TARURA wanakutana na mkandarasi kila mara wanachukua 10%, maisha yanaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muda wa kufikiria kujenga barabara za lami na tuachane na barabara za vumbi. Wamerahisisha lugha kuiita barabara za vumbi. Mzee ni barabara za vumbi wakati wa kiangazi, ikifika wakati wa masika ni barabara za tope. Nadhani tuzibadilishe jina tuziite barabara za tope.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kigoma Mjini, tulipata ufadhili wa Nchi ya Belgium mwaka 2018 mimi nikiwa Diwani. Belgium walikubali kutujengea kilometa 42 za barabara za pavement blocks ambazo zingeenda kufuta shida yote ya barabara katika Jimbo la Kigoma Mjini, lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea na mkandarasi alikuwepo, upembuzi yakinifu ulishafanywa na kila kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilienda kwa Mheshimiwa Profesa Shemdoe, nyumbani kwake, sikumkuta. Nilienda kwake sikumkuta, nikauliza hata shemeji yangu nae sikumkuta. Nilikuta watoto wake, maana niliona sura zinafanana na Profesa Shemdoe mtupu, nikajua ni watoto wake. Lengo nilikuwa ninataka nikae na Profesa Shemdoe tuongee kifamilia kuhusiana na barabara za Kigoma Mjini. Jimbo la Kigoma Mjini ndio jimbo la mjini ambalo lina barabara za vumbi kuliko jimbo lolote duniani, siyo Tanzania, dunia nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nikuhakikishie, ukienda Kata ya Mwanga Kaskazini, kuna barabara inaitwa Barabara ya Serengeti ambayo inaunganisha Kata ya Mwanga Kaskazini na Kata ya Gungu. Hiyo barabara ina makorongo ambayo ukifika Mheshimiwa Waziri Mkuu, utasema Inna lilahhi wa inna ilahhi raji'un. Ukienda Kata ya Buzebazeba, kutokea uwanja wa Lake Tanganyika, ukipita barabara hiyo ambayo inaenda ku-connect mpaka soko la Buzebazeba, ina-connect Kata ya Rusimbi, ina-connect Kata ya Kasingirima, ina-connect Kata ya Majengo, ina-connect Kata ya Machinjioni, barabara zote hizo ni vumbi tupu. Ifikie hatua watusaidie watu wa Kigoma na sisi tupate barabara ambazo zitaenda kuchochea maendeleo ya mji wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunaenda pale na Mheshimiwa Waziri Mkuu ninadhani kesho kutwa kwenda kukutana na wafanyabiashara kutoka Congo, Burundi na sehemu nyingine tofauti tofauti. Wanaenda kuona aibu iliyopo pale Kigoma Mjini. Wanaenda kushuhudia barabara za vumbi zilizotaradadi pale ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wakishaona hizo fursa, baadaye wataanza kuzinunua nyumba za wapiga kura wangu kwa bei ndogo kwa sababu nyumba iko kwenye korongo, utamuuzia nani bei kubwa? Watazinunua bei ndogo, baada ya kuja kujenga barabara, wananchi wetu watakuwa wamepoteza opportunity. Huu ni muda, wameniamini, kibarabara, mtoto wao. Nimekuja kuwaombea barabara kwa ajili ya Jimbo la Kigoma Mjini katika Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. watusaidie barabara, watupe barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tukifanya maamuzi ya pamoja Wabunge wote, ninawaambia ukweli; mama alivyokuja kuhutubia Bunge hapa, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wetu, alivyotaja tu barabara, Bunge zima likapiga makofi, akajua hapa kuna tatizo na ndiyo maana ameongeza hela kwenye upande wa barabara, lakini bado tunaomba sana utusaidie watu wa Kigoma tuweze kupata barabara. Hiyo ni tabu kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida ya pili, mafuriko. Jimbo la Kigoma Mjini limekumbwa na mafuriko. Yapo mafuriko ambayo yanatengenezwa na Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu analeta mvua nyingi, mafuriko yanatokea. Hilo hatuwezi kumlaumu mtaalam yeyote, lakini yapo mafuriko ambayo yanasababishwa na uzembe wetu sisi ambao ni viongozi tuliopewa nafasi ya kuwaongoza wale wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, sehemu ambapo maji yangefuata mtaro yangeenda ziwani moja kwa moja, hujajenga mtaro. Tafsiri yake maji yanachagua sehemu ya kupita, aidha yachague sebuleni au chumbani kisha yapitilize yaendelee na shughuli zake. Kwa hiyo, kuna makosa mengine hata mimi kwenda kuwapa watu pole ninaona aibu. Huwezi kwenda kuwapa watu pole sehemu ambapo ungejenga mtaro mkubwa, maji yasingeleta mafuriko kwenye nyumba za watu. Siwezi kwenda na nikimwona Waziri anakwenda aende yeye, wakamzomee yeye mwenyewe, mimi siwezi kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka niende na Mheshimiwa Profesa Shemdoe, twende tukazindue mitaro, tukazindue barabara, hapo tutashirikiana kwa pamoja. Ninawaomba sana, namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu atusaidie watu wa Kigoma tuweze kupata barabara, lakini pia suala la mafuriko ya Bwawa la Katubuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Bwawa linaitwa Katubuka. Hili Bwawa liko miaka yote tangu tumezaliwa, halikuwahi kufurumia kiasi kile, lakini wataalam wetu walitengeneza mitaro wakaelekeza maji yote ya mji kwenye hilo bwawa. Sasa hivi limebadilika limekuwa ni bwawa ambalo linaleta mafuriko kwenye Mji wetu wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna mtu alikuja kutudanganya siku aliyosema ni uongo au ni ukweli akasema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza shilingi bilioni nne kwa ajili ya kwenda kutengeneza mtaro wa kuyatoa maji pale Katubuka. Tukamwona mkandarasi anaanza kazi, nami nikaenda kuitisha mkutano, nikasema mnaona kazi ya mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya mwezi mmoja na nusu mkandarasi ametoa vifaa vyote anasema hana hela. Nikamuuliza shida ni nini? Akaniambia pesa nilizokuwa ninazitumia kujenga hapa ni pesa ambazo nilipewa kwa ajili ya Barabara ya kutoka Katonga kwenda Ujiji. Sasa barabara ile inatakiwa kwisha na hapa siwezi kuendelea kwa sababu hela ya huu mtaro sijapewa. Mzee wangu Prof. Shemdoe, anisaidie. Mimi ni mmoja kati ya mashabiki wake, ninamkubali, anatusikiliza, tunamheshimu, anatuheshimu na hata 2030 akichukua fomu yoyote tuko nyuma yake mzee wangu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Malizia kwa kuunga hoja.

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamalizia suala la mwisho, ni suala la fidia. Wananchi wa Kata ya Majengo pamoja na Machinjioni walikubali kupisha upanuzi wa airport pale Kigoma Mjini na wakazuiliwa baada ya kufanyiwa valuation, wakazuiliwa wasijenge tena kwenye nyumba zao kwa sababu wanasubiri kulipwa. Sasa tunakwenda mwaka wa pili; tofali liking’oka mtu anashindwa kurudishia kwa sababu anaamini kwamba hilo tofali litaongeza gharama ambayo hatalipwa. Ni muda umefika sasa twende tukawalipe wale wananchi fidia pale Kigoma Mjini ili maisha mengine yaweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kusema hayo machache, ninamalizia na hili la wavuvi mzee wangu; ninaomba Mwenyekiti wangu anisaidie Wabunge wenzangu si wanaona kama kidogo mambo ni mazuri?

MWENYEKITI: Malizia, ninaomba umalizie kwa kuunga mkono hoja, ninadhani nimekuongezea muda wa kutosha.

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawasawa kwenye suala la wavuvi, ninaunga sana mkono hoja baada ya kuona Ziwa Tanganyika ni moja ya...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chipando.

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda mrefu 2026/2027 - 2050/2051, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2026/2027 – 2030/2031) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2026/2027 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali katika Muda wa Kati ya 2026/2027 - 2028/2029